Habari kuhusu Majanga kutoka Januari, 2013
Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko
Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.
Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan
Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano...