Habari kuhusu Majanga kutoka Machi, 2010
Mwaka Mmoja Baada ya Mapinduzi, Viongozi wa Madagaska Wakabiliwa na Vikwazo
Machi 17, 2009 nchini Madagaska, vikwazo vinavyowalenga viongozi wa sasa wa Madagaska vinaandaliwa kwa kushindwa kwao kuheshima makubaliano ya Maputo ambayo hapo awali yalifikiwa na pande zote zinazohusika. Matokeo ya vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuiwa kwa mali zinazozalisha fedha na pengine kukamatwa kwa wanaohusika endapo watasafiri nje ya nchi.
Chile: Tetemeko la Ardhi Lafichua Ukosefu wa usawa Katika Jamii
Ukiukwaji sheria kulikojitokeza baada ya tetemeko la ardhi la Februari 27 nchini Chile kumezua mjadala wa kitaifa kuhusu kutokuwepo kwa usawa wa kijamii na kiuchumi nchini.
Kenya: Mafuriko Makubwa Yapasua Kingo za Mto Ewaso Nyiro Huko Samburu
Alfajiri siku ya Alhamisi, tarehe 4 Machi 2010, mafuriko makubwa yaliikumba Samburu huko kaskazini mwa Kenya na kuharibu nyumba 6 za kulala watalii watalii, baadhi ya kambi za utafiti wa...
Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia
Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.