Makala haya yamechapishwa kwa kuchelewa kutokana na sababu za kiufundi. Tunaomba radhi kwa kuichelewesha.
Matetemeko makubwa mawili ya ardhi yalilitikisa eneo la kaskazini magharibi nchini Iran, Mashariki jimbo la Azarbaijan mnamo Jumamosi (Agosti 11, 2012), na kuua watu 250 na kujeruhi karibu 1800. Matetemeko ya ardhi kipimo cha 6.4 na 6.3 katika ukubwa, na kusababisha uharibifu mkubwa na mateso.
Wa-Irani waliingia kwenye mtandao wa intaneti ili kuwaombolezea wahanga na kuomba watu kujitolea damu na msaada. Pia walionyesha hasira zao kwa televisheni ya kitaifa ya Iran, ambayo hutangaza vipindi vya dini, badala ya kutoa taarifa kwa watazamaji kuhusu matetemeko ya ardhi na jinsi ya kusaidia.
Damavandiyeh aliandika [fa]:
Watu wengi bado wako chini ya kifusi katika vijiji. Vituo vyote vinavyo endeshwa na taifa [katika Iran hakuna kituo cha kibinafsi] vina tangaza vipindi vya dini, badala ya kuwaita watu kusaidia. Mwakilishi wa Iran Koingozi Mkuu katika Mashariki ya Azarbaijan alisema tetemeko hili linatukumbusha “Siku ya Hukumu ‘.
Green City aliongeza [fa]:
Watu wako chini ya kifusi wanaohitaji msaada lakini vituo vya televisheni vya Iran vinatangaza vipindi vya dini [Dua'a Jawshan Al Kabir] na mmoja wao ni kuonyesha “Chini na Marekani’ [kaulimbiu]…
Aandishe alitafakari juu ya janga hilo,akishangaa kwa nini kamwe hawajifunzi na makoza ya uzoefu:
Kila mmoja wetu anaweza kuwa amefika katika eneo hilo… kwa nini hatuwezi kujifunza somo lolote kutokana na matetemeko ya awali … aibu kwa waongo wanaokuja kwenye Televisheni na majadiliano juu ya mafanikio yao ya kuongeza upinzani kwa majengo ya kukabiliana na matetemeko ya ardhi katika Iran.
Bidad anaonyesha [fa] hisia zile zile:
Mawasiliano yote ya simu yameingiliwa, mkoa nusu umeharibiwa na mazungumzo yote kwa televisheni ni kuhusu masuala ya dini kama vile kufunga badala ya kuhabarisha watu kuhusu tetemeko la ardhi.