Baada ya siku chache kupita nchini Madagaska, idadi rasmi ya madhara yaliyosababishwa na kimbunga kilichopewa jina la Fanele zimewasilishwa. Rais Ravalomanana alikwenda kwenye moja ya maeneo yaliathirika na kimbunga ili kutathmini madhara yaliyotokea.
Uandishi wa kiraia wakati wa kimbunga
Wakati idara inayoangalia athari na majanga, BGNRC bado haina tovuti, taarifa zinahusu madhara yaliyotokea zinakusanywa na wanablogu wawili, Marie Sophie Digne pamoja na Tomavana katika zana-huria ya Google Map.
Ufuatao ni muhtasari wa uharibifu uliotokea, kwa mujibu wa shirika la IRIN kupitia Relief Web:
Takwimu zilizotolewa na Idara Inayoangalia Athari na Majanga ya Madagaska (BGNRC) zinaashiria kwamba Kimbunga Fanele kimeua watu wanane na kuathiri watu wengine wapatao 40,400 [..]. Pia, BGNRC ilieleza kuwa watu wengine 63,000 wako hatarini huko Menabe ikiwa mvua kubwa itaendelea kunyesha. Timu za misaada bado zinaendelea kutathmini uharibifu uliosababishwa na vimbunga viwili, na takwimu zinategemewa kuongezeka wakati ripoti ya uharibifu uliotokea ikikusanywa.
Machafuko ya Kisiasa
Ulimwengu wa Blogu wa Kimalagasi kadhalika ulikuwa umeenea habari za kisiasa na maoni kuhusu maandamano makubwa leo (Januari 24) yanayotaka kufanyike kwa mgomo wa kitaifa ili kuishurutisha serikali ijiuzulu.
Wanablogu wengi wamekuwa wakiblogu moja kwa moja na kutuma picha za tukio hilo (picha nyingine zimetoka kwenye Facebook).
Bloga Ariniaina ametoa muhtasari wa mazingira yaliyopelekea kuzuka kwa machafuko hayo:
Andry Rajoelina (au Andry TVG) alikuwa na stesheni ya televisheni inayoitwa VIVA na bado anayo stesheni ya redioyenye jina hilohilo. Waziri wa Mawasiliano ameamua kuifunga stesheni ya Televisheni ya VIVA kwa sababu ya filamu iliyopeperushwa na stesheni hiyo. Ilikuwa niujumbe kutoka kwa rais wa zamani wa Madagaska, Didier Ratsiraka [..] Kutokea hapo, Meya (wa jiji la Antananarivo, Andry Rajoelina) alitoa amri ya kufunguliwa tena kwa stesheni ya VIVA kabla ya tarehe 13 Januari [..] Kwa sababu Andry hakupata kile alichokitaka, aliwaalika watu wa Tana kufanya mgomo TENA leo, tarehe 24 Januari.
(Picha ya maandamano na ariniana)
Bloga Jentilisa amnatoa upembuzi wa kina wa maelezo ya opande zote mbili za siasa na anatahadharisha dhidi ya uenezaji wa uvumi usio na hakika (mg):
Mti ulianguka katika kiwanja cha demokrasia (ambako mkutano ulifanyika) kwa sababu ya ushawishi dhahiri (ujumbe uliosikika kwenye redio); bado wengine wanadai kwamba “kulikuwa na hujuma”. Kwa hiyo, sasa tunaongelea tukio lisilo na msingi wowote. Bado tu wepesi kuamini jambo lolote tunalosikia na ningependa kuwatahadharisha dhidi ya hilo.
Bloga Avylayitra anatukumbusha kwamba serikali pia inajaribu kuitokomeza Redio VIVA na kwamba sababu inazotoa ili kuifunga haziridhishi. Kuna sheria inayokataza redio binafsi kutoa matangazo nchi nzima. Na kuna redio inayoiunga mkono serikali, Redio MBS imekuwa ikirusha matangazo nchi nzima kwa miaka 5 bila ya shaka ya kuchujwa kile inachotangaza (mg):
Sitaki kuisema MBS peke yake. Ila tu ninauliza: “Je sheria inatekelezwa kwa wachache tu?”
(Fulana ya Ndiyo Twaweza ya wanaharakati wa Kimalagasi na Avylayitra)
Historia Inajirudia
Mwanahabari na Bloga, Mialisoa Randriamampianina, anasikitika kuona matukio ya mwaka 2002 yakijirudia, yakiwa na makosa yaleyale, na maneno yaleyale ya kiburi na demokrasia iliyo mbali na ukomavu (fr):
Bila ya kuwa na utamaduni wa kweli wa kisiasa, umati unakimbilia malalamiko ya zamani ya kuonewa, kelele zinazidi na tahadhari za busara zinatoswa dirishani [..] Vivyo ndivyo tulivyofanyamwaka 2002, na vivyo tutafanya mwaka 2009 [..] Barabara ndiyo njia pekee, nguvu yetu, nia pekee mbadala. Na hatimaye kutatokea mlipuko usio na maana. Ni lazima pawe na njia ya kufikisha ujumbe, bila ya vitisho na kushushiana hadhi. Na wakati tukisubiri mitizamo ya wenye vichwa vilivyopoa, tupo hapa, tukijaribu kutafuta njia ya kutoka. Na huku ndio tulikokuita “kutafuta demokrasi”
Na pia mwanahabari/bloga, Randy, anaafiki kwamba Madagaska yawezekana kwamba bado haiko tayari kwa demokrasia ya kweli (fr):
Na hilo ndilo linalowatisha watu. Kama ilivyotokea katika nchi nyingi barani ambazo zilijaribu mchezo (wa demokrasi), maandamano ya ghafla ghafla ndiyo yalipamba jukwaa.
Cha kushangaza kwa rais wa sasa kutishwa na nguvu za umma sawa na zile zilizompandisha madarakani, hakijamponyoka bloga Rajiosy (fr):
Cha kushangaza katika habari hii ni kuwa huyu huyu huko nyuma ambaye hakutumia utaratibu wa kisheria hivi sasa amepata kazi ya kurejesha madaraka ya dola na kuimarisha vyombo vya dola. Havi sasa anakabiliwa na kazi ya kuimarisha nafasi yake. Kazi ngumu, ukizingatia kuyumbayumba kwa maoni ya wananchi.
Ulimwengu wa Twita unaokomaa
Maendeleo yenye mvuto wakati wa matukio haya ya kisiasa ni kuzuka kwa watumiaji hai wa Twita kwa Kimalagasi ambao walituma maendeleo ya kisiasa katika muda uliopo. Yeyote anaweza kufuatilia jumbe za twita zinazohusiana kwa kutafuta #madagascar: