Habari kuhusu Kiingereza kutoka Juni, 2012
Zambia Yapanga Bei ya Mahindi kwa Mara Nyingine, Yaikasirisha Benki ya Dunia
Kupanda kwa bei ya mahindi, chakula kikuu nchini Zambia kumesababisha raia kufanya ghasia na hata kusababisha jeshi kuingilia kati. Pamoja na tahadhari iliyotolewa na benki ya dunia kwamba hatua hiyo ingeathiri sekta ya kilimo, watawala wa nchi hiyo wameendelea kupanga bei ya unga wa mahindi.
Kenya: Wanaharakati wapigana vita dhidi ya ufisadi kwa intaneti
I Paid a Bribe ni njia mojawapo inayotumiwa na wanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, kwa kutumia teknolojia mpya ili kuwawezesha kupata ripoti za utoaji wa hongo.' I paid a Bribe' imefuatia muundo wa ‘India Anti-Corruption Portal (IPAB)' na ni ushirkiano kati ya IPAB na Wamani Trust ya Kenya ili kuleta IPAB katika Afrika Mashariki na Kati.
Marekani: Kumbukumbu la Walters Art lachapisha Mkusanyiko wa Picha
Jumba la Kumbukumbu la The Walters Art lililoko Baltimore, Maryland limechapisha zaidi ya picha elfu kumi na tisa kwenye mkusanyiko wa Wikimedia Commons na kuziweka chini ya leseni Creative-Commons. Jumba lenyewe lina mkusanyiko wa michoro kutoka Roma na Ulaya.
Uganda: Je, Uganda inageuka kuwa dola ya kifalme?
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Majuma machache yaliyopita, wananchi walianza kudodosa habari za nani hasa atamrithi kama ataamua kutokugombea kwa awamu ya nne mwaka 2016. Tetesi zinadai kwamba rais anamwunga mkono mkewe, Waziri wa mambo ya Karamoja kurithi kiti cha rais.
Kenya: Habari za Mlipuko Jijini Nairobi Zatawala Mijadala ya Twita
Kufuatia mlipuko mkubwa ulioathiri vibaya mtaa mkubwa wa Nairobi, Moi Avenue, wakenya na marafiki wa Kenya walitumia mtandao wa twita kuhabarishana, na kusambaza taarifa, kushauriana na kujadili tukio hilo baya.
Lesotho: Uchaguzi wa amani ambao hukuusikia
Lesotho, nchi ndogo inayozungukwa na Afrika Kusini pande zote, ilifanya uchaguzi wa wabunge Jumapili, uchaguzi ulioendeshwa kwa utulivu, lakini uchaguzi huo haukupewa uzito na vyombo vikuu vya habari.