Uganda: Je, Uganda inageuka kuwa dola ya kifalme?

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Kabla ya uchaguzi uliopita mwaka jana 2011, wapo watu walidhani kuwa asingetamani tena kugombea kwa awamu ya tatu mfululizo, lakini kinyume na matarajio ya wengi akajitokeza kugombea na hatimaye akashinda uchaguzi huo.

Baadae alinukuliwa kutamka kwamba angestaafu atakapofikisha umri wa miaka 75. Ikumbukwe kwamba awamu yake hii ya tatu itakapofikia mwisho mwaka 2016, Museveni atakuwa amefikisha umri wa miaka sabini na miwili, hiyo ikimaanisha kuwa bado anaweza kusimama kugombea awamu ya nne.

Majuma machache yaliyopita, wananchi walianza kudodosa kuhusu nani hasa anaweza kumrithi rais ikiwa yeye mwenyewe hatajitokeza tena mwaka 2016 kwa awamu nyingine ya nne.

Yoweri Museveni akiwa na baadhi ya wabunge wa Uganda katika Bunge la nchi hiyo. Picha ya ugpulse.com.

Baadhi ya majina yaliyoorodheshwa katika makisio ya watu ni pamoja na mkewe Janet Kataha Museveni, mwanae wa kiumeMuhoozi Kainerugaba, Amama Mbabazi, Waziri Mkuu na rafikiye wa karibu, na Rebecca Kadaga, spika wa sasa wa Bunge.

Tetesi zilianza kusambaa nchini Uganda kwamba Rais alikuwa akimwunga mkono mkewe Janet katika mbio za mama huyo kutaka kurithi kiti cha urais baada ya mumewe. Ndani ya muda mfupi, wa-Ganda waliingia kwenye mitandao ya kijamii kutajadili tetesi hizo.

Kwenye mtandao wa twita:
@Since__1986 alifikiri Janet Museveni amekuwa rais wa nyuma ya pazia kwa muda wote wa urais wa mumewe:

@Since__1986: Janet Museveni agombee urais? Hivi wa-Ganda wanavuta sigara gani? Huyu mwanamitindo amekuwa rais nyuma ya pazia kwa miaka 26!!! Mungu wangu mlikuwa hamjui?!

@kristinrawls akauliza:

@kristinrawls: @mjwilkerson Mna maoni gani kuhusu Museveni kumwunga mkono mkewe awe rais? Ni kitendo cha halali? Je, ataendelea kukaa ikulu?

@mjwilkerson akajibu:

@mjwilerson: @kristinrawls Ni wazi kabisa-Janetangeweza kugombea lakini ukweli ni kwamba Musevenihana tena mtaji wa kisiasa kutuamulia nani awe rais, labda kutushawishi

@shopetie_101 alifikiri Janet kumrithi rais ni dalili za ulafi:

@shopetie_101Rais wa Uganda,Yoweri Museveni anatamani mkewe, Janet Museveni kumrithi…jamani watu weusi na ulafi!

Katika mtandao wa Facebook:

Sseguya Gerald aliandika:

Mke wa ndoa wa Museveni, Janet, anataka kumrithi rais. Hawa watu hawajifunzi? Wenye busara hujifunza kwa makosa ya..

Emeruwa Nkere anapendekezaviongozi wa ki-Afrika wafanyiwe uchunguzi wa akili kwa lazima:

Rais wa Uganda anatamani mkewe amrithi pale atakapomaliza kipindi chake –Chanzo: jarida la The SUN la tarehe 31 Mei, 2012. Taarifa zilidokeza kwamba Rais Yoweri Museveni wa Uganda hawezi kuendelea zaidi ya ukomo rasmi wa umri ambao ni miaka 75. Ah! Mwuungwana wa aina yake Afrika. Lakini huyu bwana Rais anataka mkewe Janet Museveni amrithi na hakuna upinzani. Ninataka kukubalina na mtu mmoja wakati fulani aliyewahi kupendekeza kwamba watawala wa Afrika –na kwa kweli wanasiasa wote ikiwa ni pamoja na au hususani nchini Naijeria, wanaotaka kutawala walazimike kufanyiwa uchunguzi wa akili kuhakikisha utengemavu wa akili zao kwa sababu WENGI wao wanaonyesha tabia zinazowakaribia kabisa wagonjwa wa akili. Je, hukubaliani na pendekezo hili? Mie nakubaliana kabisa.

Benon M Gowa alimlinganisha Janet Museveni na wanasiasa wengine wa kike katika sehemu nyingine za dunia:

Haa, Mama Janet Kataaha Museveni (nee Kainembabazi), mke wa Rais tangu mwezi Mei 1986 ametoa hadharani wasifu wake binafsi (CV) akikwea hatua kwa hatua kutoka mama wa kupanga safari za mumewe mpaka kuwa mbunge anayewakilisha jimbo la Ruhaama, kisha Waziri wa Nchi anayeshughulikia mambo ya Karamoja (Februari 27, 2009) mpaka kuwa Waziri kamili wa masuala ya karamoja (tangu Mei 27, 2011). NA mtu yeyote anayefikiri kwa makini lazima awe na wasiwasi na ukweli uliofichwa, kwamba kwa kurejeshwa tena Ukomo wa Mihula ya Urais, basi maana yake ni kwamba itawezekana mama huyu akashawishiwa na chama kinachotawala cha NRM kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho kama ilivyokuwa kwa mwanamama Cristina Fernandez de Kirchner, rais wa sasa wa Ajentina ambaye alisimikwa na chama cha mumewe (Frente Para La Vietoria) kuchukua nafasi ya mume wake baada ya kipindi chake kumalizika ingawa mwaka 2007 chama Democrats (huko Marekani) kwa dhati kabisa walimkataa Hilary Rodmahn Clinton…

Medo Joseph alijiuliza ikiwa Afrika inaweza kuendelea katika aina hii ya “ukichaa wa ki-Afrika”:

Medo Joseph Rais Yoweri Museveni anaachia ngazi, mke wa Rais Janet Kataaha Museveni amejitokeza kuwa mrithi anayeungwa mkono na rais! UKICHAA WA KIAFRIKA! Ni lini Afrika itaendelea?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.