Kenya: Wanaharakati wapigana vita dhidi ya ufisadi kwa intaneti

I Paid a Bribe ni njia mojawapo inayotumiwa na wanaharakati dhidi ya ufisadi nchini, kwa kutumia teknolojia mpya ili kuwawezesha kupata ripoti za utoaji wa hongo.’ I paid a Bribe’ imefuatia muundo wa ‘India Anti-Corruption Portal (IPAB)’ na ni ushirkiano kati ya IPAB na Wamani Trust ya Kenya ili kuleta IPAB katika Afrika Mashariki na Kati.

I Paid a Bribe ni:

www.ipaidabribe.or.ke  ni njia ya kipekee kutoka Wamani Trust ya kupigana na ufisadi kwa kupitia nguvu za wananchi. Mtu anaweza kupiga ripoti kuhusu mifano, nambari, aina, maeneo na wingi wa vitendo vya ufisadi kwa mtandao huu. Ripoti za wananchi zitasaidia kupatiana picha ya vitendo vya ufisadi mijini. Ripoti hizo zitatumiwa kutetea uboreshaji wa mifumo na utaratibu wa serikali,utekelezaji wa sheria na hivyo basi kupunguza visa vya ufisadi mtu anapotaka huduma za serikali.

Watu wamealikwa kuandikisha hongo walizotoa na kubainisha kama walilazimishwa kutoa hongo au ni kipi kilichowafanya kutoa hongo yeneyewe. Wanauliza watu wawe huru kwa kutoa maelezo kwani majina yao wala nambari zao za simu hazihitajiki.

‘I Paid a Bribe Kenya ‘ pia ilizindua namna ya kutumia ujumbe mfupi wa simu ili kuwawezesha Wakenya zaidi ya milioni elfu ishirini na tano kuwasilisha ripoti zao.

Ili kuwasilisha ripoti zao, watu wanafaa kutuma ujumbe mfupi kwa nambari 2025 na waandike jina la kata, idara na kiwango cha pesa.

Kuna njia tatu za kuwasilisha ripoti kupitia mtandao huu:

Wakenya wanaweza kutumia intaneti (ipaidabribe.or.ke), njia ya simu (m.ipaidabribe.or.ke) au kutuma ujumbe kwa 2025 kwa shilingi tano.

Collins Baswony anaeleza njia ambayo kuwasilisha ripoti kwa mtandao itaweza kusaidini dhidi ya vita vya ufisadi:

Ufisadi mdogomdogo huwa hauripotiwi nchini.

Watu tisa kati ya kumi waliofanyiwa utafiti na East African Bribery Index 2011 walisema hawakuripoti ufisadi.

Watu wasiporipoti visa hivi vidogovidogo vya ufisadi, watumikiaji wa umma wataendelea kutumia nyadhifa zao kujinufaisha.

Ufisadi unazorotesha maendeleo ya nchi.

Gharama ya visa maarufu vya ufisadi nchini kama Golden Berg, AngloLeasing, Kashfa ya Mahindi na Mafuta, kashfa ya shilingi kwa dola ni kubwa sana. Hebu tafakari kama hizi hela zingetumika kwa kuendeleza miradi ya maendeleo.

Kenya inaendelea, mwongozo wake wa kijamii, kiuchumi na kisiasa ukiwaVision 2030. Ufisadi unabaki kuwa kizuizi kikubwa kwa mtazamio huu. Vision 2030 itabaki kuwa mazigazi kama wakenya hawatashirikiana kupigana na ufisadi.

Mgeni kwa mtandao ambaye hakutaka kutambulika ana haya ya kusema:

Kunyamaza kunazidi kuzorotesha mambo kwa kuwa hakuna anayeteta. Wakenya wamezoea kuwa sawa na hali ilivyo badala ya kujaribu kurekebisha mambo.

Kwa siku tunazoishi za teknolojia mpya na intaneti habari kama hizi zinaweza kuenezwa kwa haraka.

Jinsi watu watakavyoendelea kuongea kuhusu ufisadi, ndivyo watu wataendelea kujua kuhusu swala hili. Watu wasiwache kuongea kwani ufisadi unaharibu jamii yetu tokea ndani.

Mwingine anaongezea:

Wakenya wana tabia ya kusahausahau mambo. Watu huongea kuhusu ufisadi wakati tu wa visa vikubwa ilhali visa vidogovidogo ndio labda vinawaibia asilimia thelathini ya pesa zao, kuharibu mali ya umma, na taratibu za jamii. Itakuwa vigumu kufikia azimio la Vision 2030 iwapo watu hawatakataa ufisadi mdogomdogo.

Ufisadi huu unawaathiri maskini na watu wa kati. Nao wafisadi wa hali ya juu wanaendelea kujinufaisha

Wasiliana nao kwa Facebook na Twitter.

Ufisadi umeenea sana kati ya wanasiasa. Goldenberg ambayo serikali ilipunguza bei ya kuuza dhahabu nje ya nchi ndio kashfa iliyoendelea kwa muda mrefu na ilikuwa na gharama ya zaidi ya asilimia kumi ya kila mwaka ya pato la taifa.

*Thumbnail image courtesy of United Nations Office on Drugs and Crime.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.