makala mpya zaidi zilizoandikwa na Joyce Maina kutoka Mei, 2014
Wakati Mgogoro wa Kisiasa Ukikolea: Thailand Kufanya Uchaguzi Mwingine Mwezi Julai
Kwa sababu ya kushindwa kwa uchaguzi wa mwezi Februari kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Thailand, uchaguzi mwingine umepangwa kufanyika Julai 20. Lakini je, upinzani utasusia kwa mara nyingine?
Hong Kong: Mfanyakazi wa Ndani Apigwa Makofi, Mateke na Kulazimishwa Kufanya Kazi Masaa 21 kwa Siku
Kesi nyingine ya unyanyasaji wa mtumishi wa ndani wa kigeni imefichuliwa. Mhanga huyo Rowena Uychiat inadaiwa alilazimishwa kufanya kazi masaa 21 kwa siku (6:00 mpaka 03:00) bila kupewa siku ya mapumziko. Alidai kupigwa makofi, mateke, kutukanwa kwa maneno vibaya na nywele zake kuvutwa. Tom Grundy aliripoti tukio hilo kwa undani.
Colombia: Hatua za Kudhibiti Mashambulizi ya Kemikali
Ili kuepusha mashambulizi ya kemikali yanayowalenga hasa wanawake katika maeneo mbalimbali ya nchi, serikali ya Colombia itaanza kudhibiti [es] mauzo ya rejareja ya kemikali ya ‘chokaa’ na vitu vya kemikali kama salfa, haidrokloriki, mariati, chokaa, naitriki na sodiamu haidroksaidi, katika hali ya kimiminika na vipande RCN Radio ilitoa taarifa kwenye...
Madai ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu Wakati wa Mgomo wa Kilimo Nchini Colombia
Tovuti ya ‘kongamano la watu’ imeshutumu hadharani [es] uvunjifu wa haki za binadamu unayoendelea katika mgomo wa kilimo [es] nchini Colombia. Wanaripoti madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mikoa mbalimbali: Catatumbo na Cucuta, San Pablo-Bolívar, Sogamoso – Boyaca, Kaskazini Santander-Hacarí, Yopal-Casanare, Boyaca, Berlin – Santander, Pinchote – Santander...
Misri, Palestina, China, India, Bangladesh, Ukraine Zashinda Katika Tuzo za Bobs
Washindi wa tuzo za The Bobs 2014 zilizoandaliwa na Deutsche Welle wametangazwa! Miradi ya mtandao kutoka Misri, Palestina, China, India, Bangladesh, Ukraine walichaguliwa kama washindi na baraza la waamuzi la kimataifa. Miradi katika lugha 14 ilishiriki kwenye akundi ya Blogu Bora, Harakati ya Kijamii Bora, Mwenye Ubunifu Zaidi na Uhalisi...
Caribbean Yajiunga na Kampeni ya #BringBackOurGirls
Kama watoto wetu wangetoweka tungelipenda dunia yote kusimama na kuja kutusaidia kuwatafuta wao. Sisi … tunauliza kwamba … kwa nini mara nyingi miili ya wanawake huwa uwanja wa vita ambapo vita hupiganiwa. Hili si tatizo ambalo linahusisha mji mdogo nchini Nigeria, ni tatizo la wasichana wote kila mahali. Tillah Willah...
Venezuela: Utata na Mashambulizi Wajadiliwa kwenye Mtandao wa Twita
Wakitumia alama ashiria #UcabCaracas na #SOSColectivosDelTerrorAtacanUCAB [SOS vikundi vya kigaidi vya mashambulizi UCAB], maoni na picha ya mashambulizi kwa wanafunzi kwenye maandamano ambayo inaonekana yalitokea katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Andrés Bello [es] mjini Caracas zimeonyeshwa sana. Miongoni mwa wale wanao twiti ndani ya chuo kikuu hicho, kilchosimamisha shughuli...
#BringBackOurGirls: Taarifa Kutoka kwa Wanablogu Wenye Wasiwasi Nigeria
Wanablogu wa Nigeria wameongezea sauti zao kwa kampeni ya #BringBackOurGirls: Sisi, wanablogu wa Nigeria tuliotia saini zetu hapa chini, kwa mtazamo na wasiwasi kwa kuendelea kukamatwa kwa wasichana wa shule wasio na hatia ambao walitekwa kutoka Chibok Aprili 15, 2014. Ni maoni yetu kwamba hakuna kiasi cha kero za kijamii...
Sio Rahisi Ukiwa Mtu Mweusi Nchini Cuba
Habari mbaya kwa Wa-cuba wenye ngozi nyeusi au yenye mchanganyiko wa weusi na weupe ni kwamba hakuna taasisi huru za kisheria itawalinda kutelekezwa na serikali. Iván anaripoti kuwa watu wasio wazungu bado wanaendelea kubaguliwa nchini Cuba.