Wanablogu wa Nigeria wameongezea sauti zao kwa kampeni ya #BringBackOurGirls:
Sisi, wanablogu wa Nigeria tuliotia saini zetu hapa chini, kwa mtazamo na wasiwasi kwa kuendelea kukamatwa kwa wasichana wa shule wasio na hatia ambao walitekwa kutoka Chibok Aprili 15, 2014. Ni maoni yetu kwamba hakuna kiasi cha kero za kijamii ama dhidi ya serikali na au watu wa Nigeria unaweza kuhalalisha tendo hili la unyanyasaji dhidi ya watoto wa shule. Kwa hiyo tunalaani vikali utekaji nyara huo.
Pia walitoa wito kwa serikali yao kuchukua hatua kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wa sekondari waliotekwa nyara na magaidi wa Boko haram wanapatikana:
Sisi, pia twatoa wito kwa serikali ya Nigeria kufanya kila kilichokwenye uwezo wake, hata kama hiyo itamaanisha kushirikiana na shirika la kimataifa la usalama, kuwaokoa wasichana kutoka mikono ya wanaowashikilia kwa sasa, na kurejesha hali ya usalama katika nchi kwa haraka iwezekanavyo. Uchaguzi unafanyika mwaka ujao. Wananchi wanataka kuwa na uwezo wa kujisikia wako salama popote pale walipo. Demokrasia hunawiri vyema wakati raia wanahisi kuwezeshwa kufanya shughuli zao za kila siku bila hofu au tishio kwa maisha wala mali zao.