Am a Kenyan citizen living in Nairobi. Graduated in tourism and currently working as a Tour Operator.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Joyce Maina kutoka Agosti, 2013
Iran: Mwanablogu Aliyefungwa Jela Afanya Mgomo wa Kutokula
Hossein Ronaghi Malki mwanablogu anayetumikia kifungo cha miaka 15 jela alianza mgomo wake wa kutokula kuanzia wiki iliyopita. Kwenye mtandao wa Facebook kampeni imeanzishwa yenye lengo la kummwuunga mkono.
Makanisa Yashambuliwa Nchini Misri
David Degner aweka picha kutoka makanisa yaliyoshambuliwa na kuchomwa katika sehemu iitwayo Mallawi, Minya, Misri ya Juu hapa. Anaandika: Siku ya Ijumaa makanisa mawili katika kijiji cha Mallawi, jimbo la Minya, yalishambuliwa na kuchomwa moto. Baada ya mashambulizi dhidi ya wafuasi wa Morsy ambapo zaidi ya watu 600 walifariki, wafuasi wa Morsy walikusanyika baada...
PICHA: Makanisa Yanalia Nchini Misri
Kufuatia kuchomwa kwa makanisa, msichana mdogo katika Misri ya Juu alichora picha hii iliyonifanya nitiririkwe na machozi: pic.twitter.com/iymw3SF49R — daliaziada (@daliaziada) Agosti 15, 2013 Mtetezi wa haki za wanawake nchini Misri Dalia Aziada aliposti twiti hii baada ya makanisa kadhaa ya wakristo kuteketezwa katika maeneo mbalimbali nchini Misri kufuatia operesheni ya kikatili iliyofanywa na jeshi...
Serikali ya Uzbeki Yatafuta Namna ya Kudhibiti Wanablogu
Serikali nchini Uzbekistan inatafuta namna ya kutumia hatua kali za kudhibiti wanablogu wa nchi hiyo. Alisher Abdugofurov kwenye Registan.net anajadili sababu ya kutokea hali hii katika jamii ambayo haina wanablogu wengi wa kuanzia zoezi hilo.
China: Kisasi au Haki?
Kashfa ya ngono ya hivi majuzi inayowahusisha majaji wawili maarufu wa Shanghai iliwekwa hadharani na mfanyabiashara Ni Peiguo anayeamini kuwa mmoja wa majaji hakutoa hukumu ya haki katika kesi ya kampuni anayohusika nayo. Alichukua uamuzi wa kulipiza kisasi kufuatia hasara ya fedha kwa kumfuatilia hakimu kwa mwaka na hatimaye kufichua kashfa yake ya ngono. Mtandao...
Iran: Waziri Mpya wa Kigeni Yupo Kwenye Mtandao wa Facebook
Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini Iran lakini ndio...