Habari kuhusu China

China Yawaamrisha Vijana Kuwatembelea Wazazi Wao

  6 Julai 2013

Wiki hii, China imeanza kutumia sheria mpya inayowataka watoto waliokwisha fikia umri wa kujitegemea kuwa na mazoea ya kuwatembelea wazazi wao, hali iliyopelekea sheria hii kudhihakiwa na watumiaji wa tovuti ya jukwaa maarufu la wanablogu la China lijulikanalo kama Sina Weibo.

China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana

Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia wake. Kwa upande mwingine, maoni yaliyotokana na tukio hilo yaliukosoa unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watu wa Afrika katika biashara ya...

China Yadhibiti Habari za Maandamano Yakupinga Kujenga Kiwanda cha Kemikali

  6 Mei 2013

Wakazi wa jiji la kusini magharibi mwa China liitwalo Kunming waliingia mtaani mnamo Mei 4, 2013 kupinga mpango wa kuzalisha kemikali zenye sumu karibu na makazi yao. Vyombo vya Habari vya serikali havikutangaza habari za maandamano hayo, na katika hali ya kushangaza wafuatiliaji wa mtandaoni wamefuta habari na picha zinazohusiana na maandamano hayo kwenye mtandao maarufu wa kijamii uitwao Sina Weibo tangu Mei 4, 2013.

China Inaelekea Wapi kwa Mwaka 2013?

  29 Disemba 2012

Kadri mwaka wa 2012 unavyosogea karibu, jarida la CHINA DIGITAL TIMES limetoa muhtasari wa mabadiliko na changamoto zinazoikabili China mwaka 2013 kwa kutumia taarifa na bashiri mbalimbali za vyombo vya habari.

Maisha Binafsi ya Watawala Wapya wa China

  27 Disemba 2012

Shirika la Habari la Xinhua lilichapisha[zh] mfululizo wa wasifu wa maisha binafsi ya watawala wa juu China, ikiwa ni pamoja na picha za familia zao, ambazo ni nadra sana katika vyombo vya habari vya China. Hatua hiyo imechukuliwa na wengi kama dalili nyingine kuwa utawala mpya wa China unaweza ukawa...

China: Hatua za Kubana Uhuru wa Habari Majimboni

  15 Oktoba 2012

Jing Gao kutoka blogu ya Tofu anaeleza namna serikali ya Fuji ilivyo na mikakati michafu dhidi ya Yunnan na jinsi inavyochukua hatua za kuzuia uchapishaji wa habari zinazoweka wazi kashfa za ufisadi zinazomkabili afisa mmoja wa serikali.