Habari kuhusu China

Wa-China Wametafuta Nini Zaidi Mtandaoni mwaka 2013

  2 Januari 2014

Mtandao wa kutafutia habari mtandaoni nchini China uitwao Baidu umetoa orodha ya maneno yaliyotumika zaidi kusaka habari. Orodha ya maneno kumi yaliyotumika zaidi ni kama ifuatavyo: Hali ya Hewa Taobao (tovuti ya kufanyia manunuzi ya mtandaoni nchini China) Wu Dong Qian Kun (kitabu cha mtandaoni cha Li Hu) The Tang Door...

China: Mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha”

Sina Weibo, tovuti ya Kichina inayofanana na Twitta, imeandaa mashindano ya “Akina Mama Wanaotamanisha.” Picha za washindani zinaonyesha wazi kwamba wengi wao sio akina mama halisi. Hata hivyo, hizo picha zinatuambia mengi kuhusu uhusiano wa kijinsia nchini China. Soma mengine kwenye tovuti ya Offbeat China.

Mandela na Mao, Hawakushabihiana sana.

Jeremiah kutoka katika studio ya Granite atoa maoni yake kwenye Televisheni ya Taifa ya China, CCTV akitaka kuonesha uhusiano uliokuwepo kati ya Mandela na Mao Zedong: Mandela hakushabihiana sana na Mao. Mao alikuwa muumini wa udhanifu kama tafsiri ya neno linavyotanabaisha, mtu aliyeamini kuwa, mchakato wa utendaji wa jambo ndilo...

China: Jukumu la Baba

  2 Disemba 2013

Mtandao wa Offbeat China umeanzisha kipindi kipya na maarufu cha televisheni kinachojulikana kwa jina la “Baba, tunaelekea wapi?”. Kipindi hicho kinawakutanisha akina baba watano maarufu pamoja na watoto wao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali za nje kwa lengo la kushindana na bila ya uwepo wa wake zao. Hapa chini,...

Je, Ni Mipango Ipi Xi Anayo kwa Vyombo vya Habari Nchini China?

  21 Novemba 2013

David Bandurski kutoka mradi wa vyombo vya habari nchini China anaangalia jinsi sera ya vyombo vya habari ya uongozi mpya wa Chama cha Kikomunisti ya Kichina, hasa baada ya mkutano wa Tatu wa Plenum. Dhidi ya kinyume cha hali ya mazingira mapya ya kitaifa ya usalama wa kamati, swali la...

China: Miitikio ya Raia wa Mtandaoni Kufuatia Muswada wa Sheria ya Kurithi Kodi

  4 Oktoba 2013

Watumiaji wa mtandao nchini China walionyesha kutokuridhishwa kwao na muswada wa sheria unaopendekeza uwezekano wa kurithiwa kodi zinazoanzia yuan RMB 800,000 [yuan ni sarafu ya nchi hiyo]. Badala ya kuziba pengo la kipato miongoni mwa wananchi, watumiaji wa mtandao wanaamini kuwa sheria mpya inakusudia kuiba fedha kutoka kada ya wafanyakzi....

China: Kisasi au Haki?

  19 Agosti 2013

Kashfa ya ngono ya hivi majuzi inayowahusisha majaji wawili maarufu wa Shanghai iliwekwa hadharani na mfanyabiashara Ni Peiguo anayeamini kuwa mmoja wa majaji hakutoa hukumu ya haki katika kesi ya kampuni anayohusika nayo. Alichukua uamuzi wa kulipiza kisasi kufuatia hasara ya fedha kwa kumfuatilia hakimu kwa mwaka na hatimaye kufichua kashfa yake ya ngono. Mtandao...

Barua ya Wazi ya Kushinikiza Kuachiwa Huru kwa Mwanasheria

  24 Julai 2013

Mnamo Julai 23, 2013, zaidi ya raia 400 wa China wamesaini barua ya kushinikiza serikali ya China kumuachia huru Xu Zhiyong, ambaye ni mwanasheria mashuhuri na mpigania haki aliyekamatwa mnamo Julai 16 baada ya kushinikiza kuachiwa kwa wanaharakati pamoja na kuratibu kampeni dhidi ya uovu unaofanywa na serikali. MRADI WA...

Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China

  16 Julai 2013

Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.