Habari za Ulimwengu: Mikesha ya Mshikamano na Wanatibeti

Tangu mwanzoni mwa Februari 2012, kumekuwa na mikesha kadhaa duniani kuonyesha ushikamano na Wanatibeti [en] kufuatia mwito wa Kalong Tripa Dkt. Lobsang Sangay.Kwa vile tarehe 22 Februari ni sikukuu ya kukaribisha mwaka mpya Tibet, wanaharakati wamekuwa wakitoa wito wa duru mpya ya harakati za mshikamano.

Tamko la Lobsang Sangay linaweza kupatikana katika YouTube, na ifuatayo ni nakala ya tafsri ya Kiingereza:

A map on global vigils in solidarity with Tibetans on February 8, 2012.Ramani inayoonyesha kesha za kuonyesha ushikanamo na Wanatibeti tarehe 8 Februari, 2012.

Ever since the invasion of Tibet, the Chinese government has claimed that it seeks to create a socialist paradise. However, basic human rights are being denied to Tibetans, the fragile environment is being destroyed, Tibetan language and culture is being assimilated, portraits of His Holiness the Dalai Lama are banned, and Tibetans are being economically marginalized. Tibet is in virtual lockdown. Foreigners have been barred from travelling to Tibet now and the entire region is essentially under undeclared martial law.

I urge the Chinese leadership to heed the cries of the Tibetan protestors and those who have committed self-immolation. You will never address the genuine grievances of Tibetans and restore stability in Tibet through violence and killing. The only way to resolve the Tibet issue and bring about lasting peace is by respecting the rights of the Tibetan people and through dialogue. As someone deeply committed to peaceful dialogue, the use of violence against Tibetans is unacceptable and must be strongly condemned by all people in China and around the world.

I call on the international community to show solidarity and to raise your voices in support of the fundamental rights of the Tibetan people at this critical time. I request that the international community and the United Nations send a fact-finding delegation to Tibet and that the world media be given access to the region as well. The leaders in Beijing must know that killing its own “family members” is in clear violation of international and Chinese laws, and such actions will cast further doubts on China's moral legitimacy and their standing in world affairs.

Tangu uvamizi wa Tibet, serikali ya Uchina imedai kuwa inataka kujenga paradiso ya Kisoshalisti. Hata hivyo, Watibeti wananyimwa haki zao za kibinadamu, mazingira yao dhaifu yanaharibiwa, lugha na tamaduni zao zinapotea, picha za Mtukufu Dalai Lama zimepigwa marufuku, na Watibeti wanatengwa kiuchumi. Tibet ipo katika hali ya kufungwa kabisa. Kusafiri ili kuingia nchini Tibet kumepigwa marufuku kwa raia wa nchi ngeni, na sasa eneo lote la Tibet lipo katika hali ya sheria ya kijeshi ambayo haijatangazwa rasmi.

Nawasihi viongozi wa Uchina kusikia vilio vya waandamanaji wa kiTibet, na hao waliojichoma hadi wakafa. Hamtaweza kushughulikia malalamishi ya waTibeti, wala kurudisha Tibet katika hali ya utulivu kupitia fujo na mauaji. Njia ya pekee ya kutatua tatizo la Tibet na kuleta amani itakayodumu ni kwa kuheshimu haki za waTibeti na kwa kutumia mazungumzo. Kama mtu anayependekeza mazungumzo kwa amani, matumizi ya fujo dhidi ya Wanatibeti hayakubaliki kabisa, na inafaa kukemewa na watu wote walio Uchina na duniani kote.

Naisihi jumuiya ya kimataifa kuonyesha mshikamano na kupaza sauti kuonyesha kuwa inatetea haki za msingi za WaTibeti katika wakati huu muhimu. Naiomba pia jumuiya ya kimataifa, pamoja na Umoja wa Mataifa, kutuma wajumbe waende Tibet ili kuthibitisha ukweli wa mambo yanayoendelea huko. Zaidi ya hayo, wanahabari na vyombo vya habari kutoka kote duniani wanapaswa pia kupewa ruhusa ya kutembelea eneo la Tibet. Viongozi walio Beijing wanapaswa kujua kwamba kuwaua watu walio katika “familia moja” nao ni kukiuka sheria za Uchina na pia za kimataifa, na vitendo vyao vinatia shaka katika msimamo wa Uchina duniani na uhalali wao wa kimaadili.

Wakati naibu wa rais Xi Jingping alipozuru Marekani wiki iliyopita, wanaharakati kutoka Tibet walimsalimu Xi na kikundi cha mashabiki walioandaliwa kwa tukio hilo na habari kuhusu haki za kibinadamu nchini Uchina.

Ifuatayo ni video kutoka YouTube iliyopigwa tarehe 15 Februari mjini Muscatine, Iowa:

Wakati sherehe za kukaribisha mwaka mpya Tibet zinakaribia, wanaharakati waliopo Hong Kong wametayarisha mkesha ya mishumaa [zh] utakayofanyika nje ya afisi ya Mahusiano ya Serikali ya Uchina ili kuwaomboleza Wanatibeti waliojichoma hadi kufa ili Tibet iwe huru. Zaidi ya hayo, watu takriban 240 wamejitolea kuhudhuria tukio linalojulikana kama “Butter Lamp Pray Event” [en] kuonyesha muungano wao na Wanatibeti kwa jumla.

Nchini Tibet, kuanzia tarehe 27 Februari 2009 hadi 19 Februari 2012, Wanatibeti 23 wamejichoma ili kushinikiza uhuru Tibet, pamoja na kurudi kwa Dalai Lama. Kati ya hao, watu 15 walifariki. Chini ya mazingira kandamizi huko Tibet, kujichoma ndiyo tendo la mwisho la upinzani usiotumia fujo. Swala la Tibet linaonekana kuwa mbali nasi, lakini kama binadamu, haimaanishi kuwa hatuwezi kufanya kitu. Angalau tunapaswa kuwaombea waliofariki.

Mojawapo ya mila za Wabuda wa Tibet ni kuchoma siagi katika taa, ambayo huonyesha nuru ya hekima na kutoa pepo mbaya. Kufuata imani yao, pia sisi tutawasha taa kwa Wanatibeti wote waliojitia moto na kujichoma, na pia tutaiombea nchi ya Tibet.

*Maelezo ya Ziada: Mwandishi ameongezwa kama mojawapo ya wenyeji wa tukio la “Butter Lamp Pray Event” katika Facebook.

Picha inaonyesha maandamano ya kila mwaka yanayojulikana kama ‘Tibet Freedom March’ katikati mwa jiji la London. Ulipigwa na sinister pictures [en], na hati miliki ni ya Demotix (12/03/11).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.