· Februari, 2014

Habari kuhusu Venezuela kutoka Februari, 2014

Orodha ya Waliouawa Katika Maandamano ya Venezuela Yapatikana kwa Lugha Tano

  28 Februari 2014

Katika blogu ya Panfleto Negro [es], John Manuel Silva na Emiliana Duarte wanafuatilia orodha ya vifo vilivyotokea kufuatia maandamano yanayoendelea nchini Venezuela. Orodha hiyo -ambayo awali ilikuwa kwa lugha ya Kihispania-imetafsiriwa kwenda lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kiitaliano/a> na Kifaransa.

Caribian: Namna Vyombo vya Habari Vinavyoathiri Mitazamo

  28 Februari 2014

Venezuela na Haiti zimekuwa zikikabiliwa na maandamano ya kupinga serikali. Hata hivyo, ukuzaji wa mgogoro wa Venezuela unaofanywa na vyombo vya habari vya kimataifa na ukimya wake kwa mgogoro wa Haiti, unaibua maswali muhimu kuhusu kuyumba kwa Marekani katika kuimaisha tunu ya haki za binadamu na demokrasia. Kevin Edmonds anatoa...

Wavenezuela Waishio Mexico Wawambia Waandamanaji: “Hamko Pekeyenu”

  24 Februari 2014

Hali ya mambo nchini Venezuela yaendelea kuzorota, huku pakiwa na maandamano na mikusanyiko nchi nzima ayalisababisha vifo vya watu kumi na mamia kujeruhiwa mpaka sasa. Wavenezuela duniani kote wanaopinga serikali yao wameandaa mikusanyiko ya amani kupaza sauti zao na kuzifanya serikali za nchi wanazoishi kuelewa mwenendo wa mambo. Mexico haija...

Maandamano ya Venezuela: ‘Vyombo vya Habari vya Kimataifa: Ingilieni Kati!’

  21 Februari 2014

Mpendwa Mhariri wa Kimataifa: Sikiliza na uelewe. Hali ya mambo imebadilika nchini Venezuela usiku wa kuamkia leo. Kile kilichokuwa kinaonekana kuwa hali ya kutokuelewana iliyokuwepo kwa miaka sasa imebadilika ghafla. Kile tulichokishuhudia asubuhi hii si habari ya Venezuela uliyodhani unaielewa. Kwenye blogu ya Caracas Chronicles Francisco Toro anashutumu kutokuwepo kwa vyombo...

Kiongozi wa Upinzani Nchini Venezuela Leopoldo López Ajisalimisha Serikalini

  20 Februari 2014

Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu. López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular, alitakiwa  kujisalimisha kwa agizo la mahakama jijini Caracas kwa kutuhumiwa kuhusika na makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano  yanayoendelea nchini...