PICHA: Maandamano Yanaendelea Kote Nchini Venezuela

Protesta en Valencia, Venezuela, el 13 de febrero, 2014. Foto de Luis Turinese, copyright Demotix.

Maandamano jijini Valencia, Venezuela, mnamo Februari 13, 2014. Picha ya Luis Turinese, haki miliki Demotix.

Katika majiji mbalimbali nchini Venezuela maandamano yanayoongozwa na yaliyoandaliwa kwa kiasi kikubwa na wanafunzi hayajakoma. Waandamanaji wanadai kuachiliwa huru kwa wanafunzi waliokamatwa na vikosi vya usalama vya Venezuela. Wanafunzi hao wameungwa mkono na kikundi cha raia na hata viongozi wa upinzania, ambao nao wanadai ufumbuzi wa matatizo ya kijamii na kiuchumi yanayowaathiri sana walio wengi. 

Tangu mwanzoni mwa mwezi Februari makao makuu ya majimbo ya nchi hiyo [es] yamekuwa vituo vya maandamano ya wanafunzi ambayo, mwanzoni, yalikuwa na wito wa kudai usalama zaidi katika vyuo vikuu. Kwa nyongeza, wanasiasa maarufu wa kitaifa walikuwa wakitangaza mikutano ya mitaani [es], inayofahamika kwa jina la #LaSalida (pa kutokea), iliyokuwa imelenga “kukuza majadiliano na midahalo ili kupata demokrasia ya kuwaokoa raia na matatizo yanayolikabili taifa”.

Ilipofika Februari 2, wanasiasa hawa waliamua kuandaa siku rasmi ya maadamano ya kitaifa, wakiwaunga mkono maelfu ya wanafunzi na raia nchini kote. Matokeo ya siku hiyo yamesababisha maandamano yaliyopata umaarufu mkubwa. Majiji kote nchini humo yanaitikia mwito wa maandamano, hata ingawa mengi ya maandamano haya yameshasababisha vurugu baina ya waandamanaji na vikosi vya ulinzi.

Mitandao ya kijamii, hususani twita, imefurika picha za maandamano hayo katika kila mkoa, ikichukua nafasi ya vyombo vikuu vya habari nchini Venezuela, ambavyo kwa sasa vimefungiwa kufuatia tishio la serikali kuvipiga faini vyombo vya habari vitakavyotangaza ama kuandika habari za maandamano hayo.

Wakati wa usiku wa Alhamisi, Februari 13, mtumiaji wa twita @yirli4ny_ aliweka mtandaoni picha ya bendera yenye mita 180 iliyokuwa ikipeperushwa katika moja ya mitaa muhimu jijini Puerto Ordaz, katika mkoa wa Guayana: 

Picha ya kusisimua!

Mwandishi Mariángela González akiwa jijini Barquisimeto, katika jimbo la Lara, alifanikiwa kupata picha ya maandamano yaliyoandaliwa na wanafunzi wa masomo ya utabibu wa Chuo Kikuu kikubwa kabisa katika eneo hilo kiitwacho Universidad Centroccidental Lisandro Alvarado (UCLA):

“Watu: sikilizeni, jiungeni na mapambano;” 5:08 pm 13/02

Jijini Barcelona, jimbo la Anzoátegui, Gabriel Bastidas aliripoti kuwa maandamano ya wanafunzi yalifunga mitaa kadhaa muhimu ya jiji hilo mapema mchana wa siku ya Ijumaa, Februari, 14:

saa 9:08 alasiri, wanafunzi wanaandamana kufunga mtaa wa Intercounal.

Jijini Maracay, mji mkuwa wa jimbo la Aragua state, Mare aliripoti kuhusu wito uliosambaa mpaka usiku katika jiji hilo:

Jijini unison: mama, baba, mwungne mkono mwanao katika mapambano haya. Saa 1:07 usiku

Vijana wa ki-Venezuela wamekuwa na harakati nyingi katika jiji la Valencia, jimbo la Carabobo, kama Angel Morales anavyoripoti:

Wanafunzi katika mtaa wa Bolívar wakitembea kuelekea kweye viwanja vya Bolivar maarufu kama Bolivar Square

Kwa mujibu wa picha iliyochapishwa na José Meza (@josegremeza), jijini Maracaibo wanafunzi walikuwa wakidai mazungumzo na maafisa wa Polisi waliowasili katika viwanja hivyo kwa mijanajili ya kuandamana: 

Pilisi wanatumia nguvu kupindukia katika viwanja vya De la República, young watu wanawalazimisha kujadiliana nao. Saa 11 jioni

Miongoni mwa sababu zilizosababisha maandamano haya ni kutokuwepo kwa uasalama na hali ya vurugu , yaliyosababisha kupotea kwa maisha ya maelfu ya wa-Venezuela. Hali hii inaonekana kwenye mabango mengi yaliyobebwa kwenye mji wa Mérida, kama Sonia Camacho alivyopata picha ya tukio hilo:

bango linalogusa hisia! [Linasomeka hivi: “Ninapigania mustakabali wa mpwa wangu; majambazi wamemnyang'anya baba yake”

Na katika jiji la San Cristóbal, mji mkuu wa jimbo la Táchira state, mapambano kati ya wanafunzi wa chuo kikuu na vikosi vya ulinzi vya Venezuela bado yanaendelea. Zaidi, wananchi wa jiji hili wametoka majumbani kwako kuwaunga mkono wanafunzi hawa waliokuwa wamepatiwa hifadhi katika makao makuu ya Chuo Kikuu cha Táchira, Universidad Nacional Experimental del Táchira (UNET). Zuleik Meneses anawashukuru kwa hilo:

shukrani kwa wananchi kwa kuwaunga mkono wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho cha UNET

Mwisho, El Periodista Cívico [es] (mwandishi wa haki za raia) amekuwa akiandika habari kuhusu maandamano hayo ya kitaifa, akiweka habari mpya kuhusu waandamanaji waliokuwa wamewekwa kizuizini katika mikoa mbalimbali ya nchi hiyo. 

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.