Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu.
López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular, alitakiwa kujisalimisha kwa agizo la mahakama jijini Caracas kwa kutuhumiwa kuhusika na makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano yanayoendelea nchini Venezuela.
Maandamano makubwa ambayo López alijisalimisha siku ya Februari 18 yalikuwa yalikuwa ya amani, na wafuasi wake walipiga kelele [es] kumwuunga mkono. Twiti ifuatayo ina mkusanyiko wa picha za maandamano na pia za tukio la López kujisalimisha kwenye mamlaka za serikali jijini Caracas:
Venezuela – Marcha del 18 de Febrero http://t.co/mPTGZShdwQ via @ famorac
- Juan Arellano (@ Cyberjuan) 18 de febrero 2014
Venezuela- Maandamano ya Februari 18
Video hii [es] ilipigwa wakati López akijisalimisha:
http://www.youtube.com/watch?v=BjehYZUjWuI
Na kwenye video hii [es] unaweza kumsikia López akihutubia umati wa waandamanaji akiwa kwenye gari ya polisi lililokuwa likilindwa kwa silaha na ambalo lingempeleka kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali nchini Venezuela.
http://www.youtube.com/watch?v=FRe32qb5OMY
Mpaka toleo la lugha ya Kihispania la posti hii linaandikwa, watu walikuwa bado wako mitaani wakiandamana[es].