Majadiliano ya GV: Maandamano ya Venezuela

Venezuela inapitia katika mgogoro wa ikuchumi, kisiasa na kijamii ambao umewafanya maelfu ya raia kuingia mitaani kuonyesha kutokuridhika kwao na hali ya mambo. Kwa zaidi ya juma moja, wa-Venezuela wamekuwa wakishiriki maandamano ambayo, mpaka sasa, yamesababisha vifo nane, mamia ya majerhi na mamia wakiwekwa kizuizini. Nini hasa kinaendelea?

Katika toleo hili la Majadiliano ya GV, mahariri wetu wa Amerika ya Kusini Silvia Viñas na mimi tutafanya mazungumzo na mwandishi wa Global Voices na mwansheria wa haki za mtandaoni Marianne Díaz Hernández ambaye anafuatilia kwa karibu vitendo vya kufuatiliwa [kiupelelezi] vyombo vya habari za kiraia na mtandao wakati huu ambapo vyombo vikuu vya habari vimefungiwa kutimiza wajibu wake nchini Venezuela.

Marianne anazungumzia kuhusiana na maisha ya kawaida nchini Venezuela -namna upungufu vya chakula na madawa unavyoathirir watu, na jinsi magazeti nchini humo yalivyopunguza kurasa na kubaki na kurasa chache mpaka nne hivi kutokana na ukosefu wa karatasi. Anapendekeza vyanzo mbadala vya mtandaoni kwa minajili ya kuchunguza taarifa, ikiwa ni pamoja na Elperiodistacivico.com, wakati huu ambao kuna upotoshwaji wa taarifa na propaganda zinawakwamisha wale wanaojaribu kuelewa hali halisi ya matukio yanayoendelea.

1 maoni

  • Kiungo cha makala haya kutokea kwenye tovuti nyingine: Majadiliano ya GV: Maandamano ya Venezuela | TravelSquare

    […] Majadiliano ya GV: Maandamano ya Venezuela Venezuela inapitia katika mgogoro wa ikuchumi, kisiasa na kijamii ambao umewafanya maelfu ya raia kuingia mitaani kuonyesha kutokuridhika kwao na hali ya mambo. Kwa zaidi ya juma moja, wa-Venezuela wamekuwa wakishiriki maandamano ambayo, mpaka sasa, yamesababisha vifo nane, mamia ya majerhi na mamia wakiwekwa kizuizini. Nini hasa kinaendelea? Katika toleo hili la Majadiliano ya GV, mahariri wetu wa Amerika ya Kusini Silvia Viñas na mimi tutafanya mazungumzo na mwandishi wa Global Voices na mwansheria wa haki za mtandaoni Marianne Díaz Hernández ambaye anafuatilia kwa karibu vitendo vya kufuatiliwa [kiupelelezi] vyombo vya habari za kiraia na mtandao wakati huu ambapo vyombo vikuu vya habari vimefungiwa kutimiza wajibu wake nchini Venezuela. Marianne anazungumzia kuhusiana na maisha ya kawaida nchini Venezuela -namna upungufu vya chakula na madawa unavyoathirir watu, na jinsi magazeti nchini humo yalivyopunguza kurasa na kubaki na kurasa chache mpaka nne hivi kutokana na ukosefu wa karatasi. Anapendekeza vyanzo mbadala vya mtandaoni kwa minajili ya kuchunguza taarifa, ikiwa ni pamoja na Elperiodistacivico.com, wakati huu ambao kuna upotoshwaji wa taarifa na propaganda zinawakwamisha wale wanaojaribu kuelewa hali halisi ya matukio yanayoendelea. Imeandikwa na Solana Larsen · Imetafsiriwa na Christian Bwaya · A… Kusoma makala kamili  »  http://sw.globalvoicesonline.org/2014/02/majadiliano-ya-gv-maandamano-ya-venezuela/ […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.