Habari kuhusu Venezuela kutoka Januari, 2012
Venezuela: Ziara ya Mahmoud Ahmadinejad Yaibua Utata
Rais wa Iran, Mahmud Ahmadinejad, aliwasili nchini Venezuela Jumapili, Januari 8, katika kituo chake cha kwanza cha ziara ya ya nchi kadhaa za Marekani ya Kusini. Ziara yake imechochea miitiko mikali kweny mitandao ya kijamii, ambako watumiaji wanahoji kama uwepo wake unaweza kuwa na faida yoyote kwa taifa.
Venezuela: Mwanaharakati wa mtandaoni Luis Carlos Díaz anyanyaswa na kutishwa na “wezi wa akaunti za mtandaoni”
Kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi minne tu, mwandishi wa habari wa Venezuela na mwanaharakati, Luis Luis Carlos Díaz, amenyanyaswa kupitia akaunti yake ya Twita [1] na simu yake ya mkononi na kikundi kinachojulikana kama cha "wezi wa akaunti za mtandaoni", na ambao hutumia jina la N33 [2], na bila shaka ni kundi lilelile la watu ambao miezi michache iliyopita liliiba maneno ya siri ya akaunti za Twita na baruapepe ya karibu watu thelathini maarufu wa Venezuela, baadhi yao ni waandishi wa habari Sebastiana Barráez, Ibéyise Pacheco, mchekeshaji wa kisiasa Laureano Márquez, mwanaharakati Rocío San Miguel na mwandishi Leonardo Padrón, miongoni mwa wengine wengi.