· Julai, 2010

Habari kuhusu Mwitikio wa Kihisani kutoka Julai, 2010

Afrika ya Kusini: Dakika 67 za Mabadikio – Siku ya Mandela

Nelson Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 jela kule katika Kisiwa cha Robben, Afrika Kusini. Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Madiba (kama ambavyo wengi wanapenda kumwita huko Afrika ya Kusini) alitumia miaka 67 ya maisha yake katika kupiga vita ubaguzi wa rangi na umaskini. Jumapili hii Julai 18 2010, kutakuwa na maadhimisho ya miaka yake 92 - na pia Siku ya Mandela - siku ambayo watu duniani kote watajitolea dakika 67 ili kuifanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi kwa wote.