Habari kuhusu Ubaguzi wa Rangi kutoka Novemba, 2009
Brazil: Je, Milango ya Benki Hubaini vyuma au Rangi za Watu?
Benki nyingi nchini Brazil zinatumia milango inayozunguka yenye vifaa vya kubaini vyuma. Je, milango hiyo inatumika kama kisingizio cha kubagua watu? Video ya uandishi wa kiraia inaonyesha moja ya matukio hayo.
Finland: Suala la Lugha
Nordic Voices anaandika kuhusu ‘suala la lugha” huko Finland.
Misri: Haki ya Kijerumani kwa Marwa El Sherbini
Muuaji wa Marwa El-Sherbini, mwanamke wa Kimisri ambaye alichomwa visu mpaka kufa na muhamiaji mwenye asili ya Urusi na Ujerumani, Alex Wiens, ndani ya mahakama huko Ujerumani, amehukumiwa kifungo cha maisha, bila uwezekano wa kuachiwa mapema. Haki hatimaye imetolewa na muuaji anaadhibiwa, wanasema wanablogu wa Misri.
Marekani: Mauaji ya Fort Hood Yasababisha Kumulikwa kwa Waislamu Walio Jeshini
Shambulizi la upigaji risasi la kushtukiza lililofanywa na mwanajeshi wa Jeshi la Marekani, Meja Nidal Malik Hassan, na kusababisha vifo vya watu 13 na kujeruhi wengine 31 katika kambi ya kijeshi ya Fort Hood, jimbo la Texas, kwa mara nyingine limesababisha Waislamu nchini Marekani kumulikwa - hasa wale wanolitumikia jeshi.
Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro
Mashirika mawili tofauti nchini Israel na katika Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia vijana wa Kiarabu na Kiyahudi kuuelewa mgogoro na kujenga daraja kati yao.