Habari kuhusu Ubaguzi wa Rangi kutoka Januari, 2013
Mwanaharakati wa Pakistani Khudi Ali Auawa Katika Mlipuko wa Bomu
Mnamo Januari 10, 2013 katika jiji la Quetta lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Pakistani, watu 82 walipoteza maisha kwenye milipuko ya mabomu yaliyolenga eneo ambalo kimsingi lenye idadi kubwa ya Waislamu wa Shia jamii ya Hazara. Irfan Khudi Ali, mwanaharakati mashuhuri wa haki za binadamu ambaye bila kuchoka aliweka wazi uonevu wa kikabila unaofanywa kwa waShia wa Hazara nchini Pakistan, alifariki katika shambulio lililofuata. Kifo chake kimechochea watu kumpa heshima kwa juhudi zake kwa kuanzisha tena maandamano kupinga mauaji ya watu wa Shia nchini Pakistani.
Bangladeshi: Msichana Mwingine Mzawa Abakwa na Kisha Kuuliwa.
Kwa mara nyingine msichana mzawa ameuawa nchini Bangladesh baada ya kubakwa kikatili. Mhanga huyo, Khomaching Marma (14) alikuwa mwanafunzi wa darasa la nane. Ubakaji huu wa kikatili uliosababisha mauaji kwa mara nyingine tena umeamsha hasira na ghadhabu nchini kote. Watumiaji wa mtandao pia wanapinga vikali vitendo hivyo.