Habari kuhusu Ubaguzi wa Rangi kutoka Mei, 2009
Uchaguzi Malawi: Utabiri wa Wataalamu wa Mambo Wageuka Batili
Wakati uchaguzi umekwisha na rais aliye madarakani Bingu wa Mutharika ameshaapishwa kwa muhula wake wa pili na wa mwisho, wanablogu wa Malawi (mabloga) bado wanashangaa kuona maendeleo kinyume na utabiri...
Sri Lanka: Wanablogu Watathmini Kifo cha Kiongozi wa LTTE
Serikali ya Sri Lanka imetangaza kwa kupitia vyombo vya habari vya taifa pamoja na ujumbe wa simu za mkononi mchana leo (Jumatatu, 18 Mei, 2009) kwamba kiongozi wa Kundi linalotaka kujitenga la Wa-Tamil, the Liberation Tigers of Tamil Eelam (LTTE), Vellupillai Prabhakaran, amefariki. Salamu za rambirambi zinaashiria kwamba alikuwa shujaa kwa baadhi ya watu kadhalika wengine walimchukulia kama muuaji katili. Wanablogu wa Ki-Sri Lanka wanatathmini urithi wa kiongozi huyu wa vita na maana ya kifo chake kwa mustakabali wa Watamil na watu wa Sri Lanka.