makala mpya zaidi zilizoandikwa na Joyce Maina kutoka Juni, 2013
Uganda: Hatimaye Magazeti Yaliyofungiwa na Polisi Yafunguliwa
Uganda imeruhusu magazeti mawili kufunguliwa tena baada ya msuguano uliodumu kwa siku 11 kati ya serikali na vyombo vya habari juu ya barua yenye waliyoipata ambayo iliyoonyesha njama ya kumtayarisha mtoto wa kwanza wa Rais Yoweri Museveni kumrithi kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 27.
Tunisia: Mwanaharakati wa FEMEN Akabiliwa na Mashtaka Mapya
Wakati mwanaharakati wa FEMEN raia wa Tunisia Amina Tyler akitarajiwa kupanda kizimbani kusomewa mashitaka mapya mnamo Juni 5, chama cha Upinzani kimekosolewa kwa kukaa kimya na kushindwa kumwunga mkono binti huyo
Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi
Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.