Joyce Maina · Juni, 2013

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Joyce Maina kutoka Juni, 2013

Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?

“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza: Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka 48,  daktari wa upasuaji macho na raia wa Italia aliyezaliwa Kongo, ni Waziri mpya wa Ushirikiano katika baraza la mawaziri la Waziri...

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

  8 Juni 2013

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...

Alfabeti Hufurahisha na Kuhuzunisha Nchini Bulgaria

[…] Mojawapo ya likizo safi na takatifu zaidi nchini Bulgaria! Ni sherehe itupayo fahari ya kuwa tumetoa kitu chochote duniani! Ni likizo isiyohusiana na waasi wowote, vita, wala vurugu, ingawa hutujaza uzalendo na furaha. […] Unapotembea katika mitaa, mabango ya ugenini na maelekezo, yanazidi haya tuliyonayo kwetu kwa mbali sana...

Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano

Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa maandishi haya [en] yaliyoandikwa katika ukurasa wa kundi la Kimasedonia kwenye mtandao wa Facebook yaliyopewa kichwa cha habari cha “Waandishi wa...

Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?

Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa kufanya manunuzi miongoni mwa watumishi wa umma. Mengineyo ni uwezekano wa kupata fursa ya elimu, huduma ya maji safi, huduma...

Gwaride la Kwanza la Mashoga Nchini Lesotho

Leila Hall anablogu kuhusu gwaride la kwanza la mashoga kuwahi fanyika nchini Lesotho: Tukio hilo limeandaliwa na Kikundi cha Kutoa msaada cha MATRIX- Shirika lisilo la kiserikali la Lesotho- linatetea haki za watu kama wasagaji, mashoga, wenye hisia za mapenzi kwa jinsia zote mbili, Wanaogeuza jinsia nchini humo. Shirika hilo, ambalo lilitambuliwa kisheria mwaka...

Ukatili wa Polisi Nchini Macedonia: Miaka Miwili Baadae

Siku ya Alhamisi, Juni 6, katika kituo cha Skopje, Vuguvugu la Kupinga Ukatili wa Polisi litatimiza miaka miwili baada ya mauaji ya Martin Neshkovski, ambayo yalisababisha maandamano makubwa katika ngazi za chini kabisa nchini Macedonia katika majira ya joto ya 2011. Tukio la Facebook [mk] kuhusu ibada ya kumbukumbu linaeleza: Siku ya Alhamisi,...

Mradi wa Kumbukumbu za Kihistoria Nchini Singapore

  5 Juni 2013

Ukiwa umeanzishwa mwaka  wa 2011, Mradi wa Kumbukumbu za Singapore unalenga “kukusanya, kuhifadhi na kuhakikishia upatikanaji” wa historia ya Singapore. Zaidi ya hayo, “ina lengo la kutengeneza mkusanyiko wa maudhui ya taifa ikiwa ni pamoja na maandiko, kanda za sauti na video kwa ajili ya kuzihifadhi  katika mfumo wa kidijitali, na kuzifanya...