Habari kuhusu Vijana kutoka Novemba, 2009
Afrika Kusini: Kikaragosi Kiliochoathirika na VVU Kwenye Kipindi cha Sesame Chaelimisha Kuhusu Ukimwi
Wakati kipindi cha watoto cha Mtaa wa Sesame (Sesame Street) kikisherehekea maadhimisho ya miaka 40 mwezi huu, kwa kizindua msimu wake mpya leo, kikaragosi kizuri kinachovutia cha Muppet katika toleo la Afrika Kusini kinaendelea kusaidia kupambana na kuelimisha kuhusu VVU/UKIMWI.
Azerbaijan: Baada ya Hukumu ya Wanablogu wa Video
Siku chache baada ya hukumu ya vijana wanaharakati wawili wa blogu za video huko Azerbaijan, wanablogu wengine wanaanza kuongea kwa sauti juu ya kifungo cha Adnan Hajizade na Emin Milli....
Vijana wa Kiyahudi na Kipalestina Watumia Video Kuuelewa Mgogoro
Mashirika mawili tofauti nchini Israel na katika Majimbo ya Palestina yanatumia zana za video ili kuwasaidia vijana wa Kiarabu na Kiyahudi kuuelewa mgogoro na kujenga daraja kati yao.