Habari kuhusu Vijana kutoka Machi, 2010
Pakistani: Vitendo vya Unyanyasaji Watoto Vyaongezeka
Msemo 'Unyanyasaji watoto' hutumika kueleza vitendo vya aina mbalimbali vilivyo jinai na vinavyofanywa dhidi ya watoto. Wanablogu wanajadili vitendo hivi vya unyanyasiaji watoto vinavyokera na vinavyozidi kuongezeka nchini Pakistani.
Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma
Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.
Moroko: Wafanyakazi wa Shirika la Misaada La Kikristu Wafukuzwa
Wiki iliyopita, wafanyakazi 20 wa Kijiji cha Matumaini, makazi madogo ya yatima katika mji mdogo wa Moroko vijijini, waliondolewa (walifukuzwa) nchini bila onyo, kwa madai ya kuhubiri dini.