Habari kuhusu Maendeleo kutoka Disemba, 2009
Misitu ya Madagascar Inateketezwa kwa $460,000 kwa Siku
Wakati mataifa ya dunia yanakutana huko Copenhagen kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, Madagascar, ambayo imekwishapoteza 90% ya misitu yake ya asili, inakabiliwa na tishio la biashara ya magendo ya magogo, inayotishia kuharibu kile kilichobakia katika moja ya mifumo ya mazingira yenye viumbe na mimea mingi inayotofautiana.
China: Uvunjaji Nyumba kwa Kutumia Mabavu
Visa viwili vya uvunjaji nyumba kwa mabavu vimeibua hisia za kutaka kulindwa zaidi kwa haki za raia na utatuzi wa migogoro nchini Uchina. Watumiaji wa mtandao wa Kichina wanatoa maoni.
Ghana: Nani atanufaika na mafuta?
Wakati Kampuni ya mafuta ya Uingereza Tullow Oil ilipotangaza uvumbuzi wake wa kiasi cha mapipa milioni 600 ya mafuta nchini Ghana mwaka 2007, ulimwengu wa wanablogu uliitikia kwa maoni yanayotofautina kati ya matumaini na hali ya hofu hasi.
Nyenzo ya Mtandaoni ya Kufuatilia Mabadiliko ya Tabianchi
Kuelekea kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya TabiaNchi utakaofanyika Copenhagen (COP15) mwezi Desemba 2009, zifuatazo ni baadhi ya nyenzo za mtandoni za kufuatilia mabadiliko ya Tabia Nchi.