Habari kuhusu Maendeleo kutoka Septemba, 2008
Msumbiji: Mgogoro wa Kisiasa Katika Jimbo la Kati la Beira
Waunga mkono wa Renamo wenye hasira walimwagika katika mitaa ya Beira ili kupinga uamuzi wa chama wa kumbadilisha Meya aliyeko madarakani Bwana Davis Simango na kumuweka Manuel Pereira kama mgombea wa kiti cha serikali ya manispaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Mwezi Novemba 2009. Mwanahistoria Egidio Vaz anaandika barua ya wazi kwa Rais wa Renamo, Bwana Alphonso Dhlakama katika blogu yake.
Venezuela: Wahindi wa Yukpa, Chavez na Mgogoro wa Ardhi
Picha za video zinazotumwa kwenye mtandao wa internet na vyombo vya habari vya kiraia zinaonyesha yale yanayojiri kuhusu mgogoro unaoibuka nchini Venezuela kati ya Wahindi wa jamii ya Yukpa wanaoishi katika milima ya Perijá, wamiliki wa ardhi na Rais Chávez. Mgogoro huu kuhusu mipaka ya ardhi umekuwapo kwa takribani miaka 30, yaani tangu pale vikosi vya jeshi vilipowandoa kwa nguvu wanajamii wenyeji ya Ki-Yukpa na kuwapa ardhi hiyo wamiliki wapya walioanzisha mashamba makubwa ya mifugo, hasa ng'ombe, ambao wameendelea kuitumia ardhi hiyo tangu wakati huo.