Habari kuhusu Maendeleo kutoka Aprili, 2011
Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi
Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.
Saudi Arabia: Mfalme Awaahidi Wananchi wa Saudia Fedha Zaidi
Fedha zaidi zimeahidiwa kutolewa kwa wananchi wa Saudia, ahadi ambayo Mfalme Abdulla ameitoa kupitia hotuba yake kwa taifa leo. Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi, Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu aliwashukuru viongozi wa dini, waandishi na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa juhudi walizofanya kutetea ufalme. Matamko na Amri vilifuata ya kwamba mabilioni yatagawanywa kwa watu wa Saudia.