Habari kuhusu Maendeleo kutoka Julai, 2010
Niger: Njaa ya Kimya Kimya
Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005.
Angola: Hapo Zamani za Kale Katika Roque Santeiro
Maendeleo yanayoukumba mji wa Luanda unaliwajibisha moja ya eneo la biashara linalotembelewa zaidi mjini humo, eneo ambalo hutengeneza maelfu ya dola kwa siku. Soko la Roque Santeiro limo mbioni kufunga "milango" yake na kufunguliwa katika eneo la kisasa na lenye hadhi, huko Sambizanga.