Angola: Hapo Zamani za Kale Katika Roque Santeiro

Picha ya soko mjini Luanda na mtumiaji wa Flickr BRamirez37, CC

Soko la Roque Santeiro, jina ambalo linatokana na maigizo maarufu ya filamu ya Brazil ambao ulipata umashuhuri miongoni mwa wapenzi wa maigizo ya filamu wa Angola, linajulikana kwa kuwa soko kubwa zaidi ya yote barani Afrika, na kwa kufanya biashara ya maelfu ya dola kwa siku, na kwa kuwa ulingo mkuu wa mauzo ya kila bidhaa inayofikirika. Kwa bahati nzuri au mbaya, siku za zoko hilo zinahesabika. Serikali ya Luanda inapanga kulihamisha soko hilo kutoka Sambizanga kwenda panguila, Karibu kilomata 30 kaskazini mwa Luanda. Tarehe bado haijaamriwa.

Soko la Roque Santeiro, liliwekwa kwenye eneo lake la sasa mnamo miaka ya 1980, wakati ambao nchi ilikuwa bado imeharibiwa na vita na mahitaji yalipokuwa adimu. Mwanzoni lilianzishwa kama vile soko la Boa Vista, eneo la biashara lilikuwa pengine ndio sehemu pekee ambayo palikuwa na uwezekano wa kupata bidhaa zozote – japokuwa kwa njia za vificho, pamoja na bunduki na biashara ya silaha na pia huduma za ngono za watu wazima pamoja na watoto.

Hivi sasa soko la Roque Santeiro ni njia ya kujikimu ya familia nyingi za WaAngola. Wakati huo huo, soko hilo pia ni hifadhi ya wahalifu ambao wanalipa eneo hilo la biashara jina baya.

Katika makala ya zamani kwenye blogu, iliyopewa jina la Angola Drops, mwanablogu wa kiBrazili analilezea [pt] soko hilo:

Fui com dois colegas brasileiros e um angolano ao mercado do Roque Santeiro que tem a fama de ser o maior do mundo. São 500 campos de futebol numa área de um quilómetro de comprimento por 500 metros de largura, que abriga cinco mil vendedores. A infra-estrutura é mínima: em todas as “lojas” o chão é o barro nu e o máximo de cobertura são telhas gastas de zinco ou mais comumente, lona. Obviamente vende-se de tudo. Logo na chegada passámos por géneros alimentícios de vegetais comercializados directamente sobre panos no chão, a enlatados, caldo de carne, maionese e alimentos prontos, principalmente banana da terra na grelha. Se o Roque Santeiro é um grande centro comercial a céu aberto, não poderia faltar o cinema. O complexo tem duas salas, erguidas com madeira e restos de lona e com capacidade para umas 50 pessoas cada. Em cartaz, Sete Vidas com Will Smith, exibido numa televisão de 29 polegadas colocada numa mesa alta. O barracão é adequadamente escuro e os espectadores vêem o filme em bancos de madeira sem encosto.

Nilikwenda kwenye soko la Roque Santeiro na wenzangu wawili wa kiBrazili na mmoja wa kiAngola, soko ambalo ni maarufu kwa kuwa soko kubwa zaidi duniani. Lina ukubwa wa viwanja 500 vya mpira wa miguu ndani ya eneo la kilomita moja kwa kilomita moja na nusu, lenye wachuuzi 5,000. muundo mbinu wake ni wa hali ya chini: kila ‘duka’ lina sakafu ya vumbi, na mapaa mazuri zaidi ni ya bati za zamani zilizochanika-chanika, japokuwa mapaa yaliyozoeleka zaidi ni ta turubai, Wazi, unaweza kukuta kitu chochote kinachoweza kuuzwa. Pale pale mlangoni tulizipita bidhaa za mboga mboga zinazouzwa moja kwa moja juu ya vitambaa vilivyotandazwa sakafuni, bidhaa za kwenye makopo, mchuzi wa nyama, achari na vyakula mabvyo viko tayari kwa mlo, hasa ndizi za kubanika. Na kwa kuwa soko la Roque Santeiro ni kituo wazi cha biashara, bila ya shaka halihitaji jumba la sinema. Jumba la sinema lina vyumba viwili vikubwa na vimejengwa kwa mbao pamoja na vipande vya turubai, vina uwezo wa kuchukua watu 50 kila kimoja. Filamu inachoza sasa ni ile ya Seven Pounds ya Will Smith katika skrini ya inchi 29 iliyowekwa kwenye meza kubwa. Hema lilizodi ukubwa lina kiza cha kutosha, na watazamaji wanaangalia wakiwa wameketi kwenye mabenchi ya mbao yasiyo na viegemeo.

Picha ya soko la Roque Santeiro na Menina de Angola

Shukrani kwa maendeleo yanayosambaa mji mzima kama moto, Soko la Roque Santeiro litaingia kwenye aya mpya ambayo ni wazi inawakera wachuuzi ambao wanakwenda pale kila siku kuuza bidhaa zao. Wazo la serikali la kulihamisha soko hilo kwenda kwenye sehemu nyingine ya mji ni sehemu ya mpango wa kuupanga upya mji wa Luanda, ili kuufanya mji huo uwe wa kisasa zaidi na salama kwa raia wake. Hivi ndivyo muandishi wa blogu ya Menina de Angola [Msichana kutoka Angola, pt] anavyoiona hali:

O mercado mais famoso do mundo vai acabar. Finalmente o governo vai transferir todos os vendedores para a Panguila, numa área organizada, com restaurantes, bancos e o mais importante condições sanitárias adequadas. Essa transferência faz parte do programa do governo de requalificação do Sambizanga que vai transformar o perigoso e violento bairro num moderno distrito comercial e residencial, com muitos prédios modernos e caríssimos.

Soko maarufu zaidi duniani linelekea mwisho wake. Hatimaye, serikali itawahamisha wachuuzi wote kwenda panguila, katika eneo lililopangwa vizuri, na migahawa, benki pamoja na, muhimu zaidi, mazingira ya usafi yaliyo sawa. Uhamishaji huu ni sehemu ya programu ya serikali ya kuiboresha Sambizanga, programu ambayo itaibadilisha sehemu hii hatari na yenye vurugu kuwa wilaya ya kisasa ya biashara yenye majengo mengi ya kisasa nay a gharama kubwa.

Piucha ya wanawake wa kiAngola sokoni Roque Santeiro, na Yan Boechat, CC

Mwandishi wa blogu ya Morro da Maianga anaorodhesha [Bonde la Maianga, pt] baadhi ya mambo yanayoweza kutokea kutokana na kufungwa kwa soko hili maarufu zaidi:

mais miséria/exclusão social/mais zunga/caos urbano/mais delinquência/criminalidade/violência/mais instabilidade/insegurança/e mais um espaço de especulação imobiliária.

Taabu zaidi/ubaguzi wa kijamii, uuzaji holela mitaani/vurugu za mjini, uhalifu/fujo, mazingira yaziyo imara/ukosefu wa usalama, na nafasi kubwa zaidi kwa ulanguzi wa maeneo ya ujenzi.

Mwisho ni mwa makala, mwanablogu huyo anaonya:

depois não responsabilizem (apenas) a polícia.

Baada ya yote, (na sio tu) polisi watajivua jukumu.

Pamoja na kutoridhika kwa wachuuzi kwa kutakiwa kuhamia sehemu nyingine, ambayo inasemekana kuwa ya kisasa zaidi, utawala wa soko unaamini kuwa uhamishaji huo utakuwa wa amani.

Ili kuiona sehemu ambayo soko jipya litajengwa, nenda kwenye: http://www.youtube.com/watch?v=sq1n72IYnzI

Makala hii ilitafsiriwa na Melissa Mann.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.