Habari kuhusu Maendeleo kutoka Juni, 2013
Simu za Bure Kwa Wakulima wa Nigeria?
Wizara ya KIlimo nchini Naijeria imetangaza mpango wake wa kugawa simu za bure za kiganjani kwa wakulima wa vijijini. Mpango huu umezua mjadala mzito kwenye ulimwengu wa blogu nchini Naijeria.
Bajeti ya Bangladesh: Maoni na Uchambuzi
“Bajeti ya kifahari lakini mpango duni?” Raia wa kawaida anatoa maoni na kuichambua bajeti ya hivi karibuni ya Bangladesh kwa mwaka wa fedha 2013-2014.
Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela
Kuhukumiwa kwa wafanyakazi wa ki-Misri na kigeni wanaofanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) kifungo cha hadi miaka mitano jela, kumesababisha hasira katika mitandao ya kijamii na katika maeneo mengine. Hatua hiyo imeonekana kama onyo kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale yanayokuza demokrasia.
China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana
Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia...
Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?
Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa...