Nyenzo ya Mtandaoni ya Kufuatilia Mabadiliko ya Tabianchi

Kuelekea kwenye Mkutano wa Mabadiliko ya TabiaNchi utakaofanyika Copenhagen (COP15) mwezi Desemba 2009, hizi ni baadhi ya nyenzo za mtandoni za kufuatilia mabadiliko ya Tabia Nchi. Kwa kutumia vyenzo hizi, watu wa kawaida wanaweza kujifunza zaidi kuhusu athari, na kusaidia kuwashinikiza wanaofanya maamuzi kushughulikia utatuzi.

Katika Viwanja Husika

Kufuatilia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ujumla huanzia kwenye viwanja husika. James Balog, mpigapicha, amekuwa Alaska, Marekani, kurekodi muda unaotumiwa na barafu kuyeyuka. Unaweza kutazama matokeo mazuri ya upigaji picha wake katika video hii hapa:

Kama huna kamera ghali na muda wa ziada kusafiri mapaka Alaska, namna nyingine unayoweza kuitumia ni kusoma uzoefu wa watu walio mstari wa mbele.

Mstari wa mbele kwenye Mabadiliko ya Tabia Nchi
ni mradi unaokusanya habari mama kuhusu athari za tabia nchi, katika jamii za wazawa, kwenye visiwa vidogo, na jamii nyingine zenye hatari ya kuathirika. Majukwaa hayo yana idadi kubwa ya michango ya hivi karibuni kwa njia ya barua pepe, nyingi zikitokea Asia kusini na Afrika. Mchangiaji mmoja na Mshauri wa maendeleo ya Afrika, George Katunguka anaandika kutoka Uganda:

Athari za mabadiliko ya tabia nchi hazijapewa kipaumbele kinachostahili katika nchi yangu Uganda lakini mabadiliko hayo na athari zake zinahisiwa kwa uchungu. Mwaka 2025, Uganda inaweza kukabiliwa na ukosefu wa maji kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni kuhusu vyanzo vya maji. Watu wanakufa kwa kukosa chakula na njaa kama ilivyokuwa hivi karibuni katika mkoa wa Teso, Mashariki ya Uganda; kuna mabadiliko katika mfumo wa wa maji kama kupungua kwa kina cha maji cha Ziwa Victoria ; majira yasiyotabirika, kupungua kwa rutuba ya udongo na kupotea kwa uzalishaji wa kilimo na hivyo kuongezeka kwa umasikini wa familia na madhara yake. Tunafanya nini kubadilisha janga hili linaliotutishia?

Kutoka anga la mbali mpaka Google Earth

Uchunguzi kutoka kwenye konde unaweza kuangaliwa mara mbili kutoka kwenye uwanda wa juu. Anga za mbali ni mahali ambapo kutokea hapo tunaweza kuichunguza na kuiainisha dunia kwa ujumla. Ni vigumu kupata kiti katika vyombo vinavyovinjari anga za mbali, lakini kwa bahati, ni rahisi kupata picha za setilaiti zinazopigwa kutoka juu angani.

Picha za setilaiti za Bahari ya Aral, Kazakhstan na Uzbekistan 1973/2004

Picha za setilaiti za Bahari ya Aral, Kazakhstan na Uzbekistan 1973/2004

Pamoja na mashirika na makapuni ya anga za juu kutoa huduma zao kwa asasi zisizokuwa za kiserikali, wanasayansi na watu wa kawaida, Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa umetengeneza kitabu cha ramani cha mtandaoni kitakachokuwa na faharasa ya mabadiliko yanayotokea kwenye maeneno mbalimbali ulimwenguni kwa miongo mingi. Picha zote za setilaiti zinaweza kuangaliwa kwenye tufe yakini ya Google Earth, kama blogu yao rasmi inavyotaarifu:

Kwa ushirikiano na serikali ya Denmark na nyingine, tunazindua mfululizo wa tabaka na ziara ili kukusaidia kuvinjari athari zinazoweza kuipata sayari yetu na ufumbuzi wa namna ya kuzidhibiti athari hizo.

Rasilimali nyingine zaidi zinaweza kupatikana kwenye blogu na tovuti za mashirika ya kimataifa. Wasomaji, jisikieni huru kuongeza rasilimali zenu kwenye sehemu ya maoni.

Sayansi kwa wanaofanya maamuzi

Uchunguzi ni suala mtambuka kwa wafanya maamuzi. Serikali zinaanzisha tafiti ili kuelewa hali hii na jinsi ya kupunguza athari.

Tume ya Ulaya na Shirika la Anga za Mbali la Ulaya zilianzisha mpango mwaka 1998 ulioitwa Uchunguzi wa Ulinzi na Mazingira wa Dunia (GMES), ili kuchora michoro inayoonesha mabadiliko halisi yanayotokea kwa kutumia takwimu zinazotoka mahali mbalimbali. Mradi unatarijiwa kutoa taarifa mwaka 2014, pamoja sehemu ya usalama.

Nchi zinzoendelea zilizoathiriwa moja kwa moja na mabadiliko ya tabia nchi, zimechukua hatua zinazofanana na hizo kama vile kuzinduliwa hivi karibuni kwa setilaiti ya India ili kujifunza mabadiliko ya tabia nchi. Taarifa kama hizo zinaweza kuzisaidia nchi kupanga sera mpya za mazingira na uchumi.

Nchini Afrika Kusini, nyenzo mpya yenye mwelekeo wa kiuchumi imetengenezwa kwa kusudi hili hili. AllAfrica inataarifu:

Sasa, nyenzo ainisho iliyotokana na utafiti, inayochora ramani ya uathirikaji wa sekta ya kilimo Afrika Kusini uliotokana na mabadiliko na kugeuka geuka kwa tabia nchi, imeundwa kuwasaidia watengeneza sera kutambua jamii ambazo zimo katika hatari ya kuathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi na kuzisaidia kujiandaa kwa namna tofauti za ukulima.

2 maoni

 • HANUSA OMARY

  Napenda kuchukua nafasi hii kujiunga katika safu hii ya mabadiliko tabia nchi hasa ikizingatiwa kuwa tishio kubwa litakuja kujitokeza katika miaka ijayo kwa kuwepo ukame anbapo hakutakuwa na njia za kurudisha hali ya zamani.
  Nchi zinazoendelea zinahitajika kuwa na busara kwa kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa ambayo inatokana na uchomaji mafuta pamoja na uchonaji wa gesi.
  Katika miaka ijayo kutakuwa na ukame wa ajabu hasa ikizingatiwa hali ya hewa inakwenda inabadilika kila miaka.

  HAMISA OMARY.
  Mwandhishi wa habari kutoka gazeti la CHANGAMOTO Lililopo jijini Dar Es Salaam.

 • HAMISA OMARY

  Napenda kuchukua nafasi hii kujiunga katika safu hii ya mabadiliko tabia nchi hasa ikizingatiwa kuwa tishio kubwa litakuja kujitokeza katika miaka ijayo kwa kuwepo ukame anbapo hakutakuwa na njia za kurudisha hali ya zamani.
  Nchi zinazoendelea zinahitajika kuwa na busara kwa kupunguza uzalishaji wa gesi ukaa ambayo inatokana na uchomaji mafuta pamoja na uchonaji wa gesi.
  Katika miaka ijayo kutakuwa na ukame wa ajabu hasa ikizingatiwa hali ya hewa inakwenda inabadilika kila miaka.

  HAMISA OMARY.
  Mwandhishi wa habari kutoka gazeti la CHANGAMOTO Lililopo jijini Dar Es Salaam.

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

 • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.