Habari kuhusu Video kutoka Aprili, 2014
VIDEO: Wanafunzi wa Iran Wavuruga Hotuba ya Mgombea Urais wa Chama Tawala
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Amirkabir kilichopo mjini Tehran, nchini Iran waliimba nyimbo zenye vibwagizo vinavyomwuunga mkono Mir Hussein Mousavi na Mehdi Karroubi, ambao ni viongozi wa vyama vya Upinzani nchini humo waliowahi kuongoza maandamano ya Green Movement.
Mazungumzo ya GV: Moja kwa Moja kutoka Kombe la Dunia la Mtandaoni
Je, tuna mpango wa utawala wa mtandao wa intaneti duniani? Mazungumzo ya wiki hii yanakujia kutoka kwenye mkutano wa Net Mundial jijini São Paulo, Brazil.
M-Misri Atumia Mtandao wa YouTube Kupinga Kutumikia Jeshi kwa Lazima
Mwanaharakati wa Misri ametumia mtandao wa YouTube kuelezea anavyopinga utaratibu wa kulitumikia jeshi kwa lazima kwa raia wenye umri wa miaka kati ya 18 na 30. Katika barua pepe aliyoituma kwa Global Voices mtandaoni, Adam anaandika: Mimi ni Mmisri mwangalifu ninayepinga kwa nguvu zote utaratibu wa kulitumikia Jeshi la Misri...
Mazungumzo ya GV: Nini Kimewakuta Wanablogu wa Iran?
Huenda kublogu hakujafa, lakini kuko mbioni? Arash Kamangir na Laurent Giacobino wanatuletea utafiti wa kina kuhusu hali ya blogu mashariki ya kati.
Unapenda wimbo gani wa kulalia?
Nyimbo la kulalia si tu zinawafaa watoto, lakini pia zinaweza kuwafaa watu wazima. Tuma wimbo wako wa kulalia kwa PRI
Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba
Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo. Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka...
VIDEO: Wimbo wa ‘Furaha’ wa Pharrell Williams na Taswira Halisi ya El Salvador
Wananchi wa Salvador wametengeneza toleo lao la wimbo “Happy” [furaha] ulioimbwa na Pharrell Williams. Mwanablogu Mildred Largaespada anaisifu video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook [es]: ni nzuri. Na ndiyo, kama ilivyo kwenye maisha halisi, video hii ni halisi: wakati mwingi wa siku, wanawake na wanaume wa El Salvador wanaoneka...