Habari kuhusu Video kutoka Aprili, 2012
Ajentina: Dokumentari Kuhusu Wenyeji wa Mjini Yatafuta Tafsiri ya Maandishi
Dokumentari iitwayo Runa Kuti iliyoshirikishwa katika mradi wa Haki miliki wa “Creative Commons” kuhusu kutambuliwa kwa wananchi waliotokana na uzao wa wenyeji wa zamani walioishi mjini katika jiji la Buenos Aires, inatafuta watu wa kujitolea kusaidia kuiwekea video hiyo tafsiri ya maandishi kwenda katika lugha za asili za Ajentina kama ki-Quechua, ki-Aymara, -kiMapuche na ki-Guaraní pamoja na ki-Kiingereza.
Tunisia: Miitikio Tofauti Kufuatia Kuingiliwa kwa Barua Pepe za Waziri Mkuu
Mnamo Aprili 8 “Anonymous Tunisia” kikundi kisichotambulisha majina ya wanachama wao nchini Tunisia (ambacho kinadai kuwa na uhusiano na kikundi cha watu “wasiojitambulisha” ) waingiliao mawasiliano ya watu kiliingilia mawasiliano the ya barua pepe ya waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali. Vuguvugu hilo lilipewa jina la utani la (“Achana na Tunisia yangu”) ambayo ni sehemu ya kampeni kuu iitwayo “Operesheni Rejeza Tunisia”.
Uganda: Ndiyo Tunampinga Kony!
Kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayokusudia kuongeza uungwaji mkono wa harakati za kumkamata kiongozi wa waasi wa ki-Ganda na mhalifu anayetafutwa kwa udi na uvumba Joseph Kony imechukua sura nyingine.
Mali: Raia Washtushwa na Mapinduzi ya Kijeshi
Askari walioasi wametangaza kwamba wanatwaa madaraka nchini Mali, baada ya kuwa wameteka nyara kituo cha televisheni ya taifa pamoja na ikulu. Wanadai kwamba serikali ilishindwa kuvipa vikosi vya jeshi la nchi hiyo msaada ili kuwakabili vilivyo wapiganaji wa kabila la Tuareg waliokuwa wakiteka miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Tanzania: Mwigizaji Nyota wa Filamu, Steven Kanumba, Afariki Dunia
Tanzania ilimuaga mmoja wa wasanii wake maarufu na nyota wa tasnia ya filamu, Steven Kanumba, kwa maziko yaliyogubikwa na majonzi mazito mnamo tarehe 11 Aprili 2012. Alifariki alfajiri ya Jumamosi, akiwa na umri wa miaka 28, baada ya kile kilichodaiwa kuwa ugomvi wa kimapenzi na rafiki yake wa kike aitwaye Elizabeth Michael kwa jina maarufu “Lulu”.
Congo (DRC): Video zasaidia kumtia hatiani Thomas Lubanga kwa uhalifu wa kivita
Mnamo tarehe 14, Machi, mahakama ya kimataifa ya makosa ya kivita ilimtia hatiani Thomas Lubanga, kiongozi wa zamani wa waasi Kongo (DRC) Mashariki, kwa kosa la kuwatumia watoto katika vita. Jaji alisema picha za video zilizoonyesha mahojiano na askari hao watoto ziliziongeza uzito wa ushahidi ulioisaidia mahakama kutoa hukumu.
Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”
Mnamo tarehe 2 Aprili, Televisheni ya Ukraine ya TVi ilirusha filamu iliyotayarishwa na Kostiantyn Usov kuhusu hali ya maisha na jinsi mahabusu wanavyotendewa katika gereza la Kyiv la Lukyanivska, na pia kuhusu kuenea sana kwa rushwa miongoni mwa askari magereza. Kwa uchache, wengi katika wale ambao tayari wametazama video ya Usov walishtushwa sana na yale waliyoyaona.