Habari kuhusu Video kutoka Aprili, 2011
Kenya: Uanahabari wa kiraia wa Mtandao wa Habari wa Kibera
Vijana wa Kibera, Kenya, kitongoji ambacho kinajulikana kwa baadhi kama eneo kubwa la hovyo zaidi ya yote barani Afrika, wamedhamiria kuonesha sura nyingine ya mahali wanapoishi. Huku wakiwa na kamera mkononi, wanavinjari mitaa kutafuta habari kuinesha dunia jinsi Kibera inavyojiona yenyewe.
Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi
Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.
Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo
Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.
Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana
Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.
Ivory Coast: Je, nani anadhibiti televisheni ya taifa ya RTI?
Bado kuna mkanganyiko kuhusu swali la nani hivi sasa ndiye mwenye udhibiti wa Radio Télévision Ivoirienne (RTI) , ambacho ni kituo cha televisheni ya taifa.
Japani: Tsunami yaathiri eneo la pwani, yaacha kila kitu kimeharibiwa
Kufuatia tetemeko kubwa kuwahi kutokea nchini, Japani imekumbwa na tsumani mbaya zaidi iliyowahi kutokea. Watu wengi nchini kote wameganda kwenye luninga zao wakati vipande vya habari vinavyoonesha tsunami lenye urefu wa zaidi ya mita 7 kwenda juu likisomba magari na majengo.