Habari kuhusu Video kutoka Disemba, 2011
Dondoo za Video: Maandamano, Chaguzi, Utamaduni na GV
Baadhi ya habari za kuvutia za Global Voices na video za hivi karibuni kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki na Ulaya Kati, Karibeani pamoja na Marekani ya Kusini, zimeletwa na Juliana Rincón Parra.
Global Voices: Changia Leo
2011 umekuwa mwaka usio wa kawaida katika maudhui ya mtandaoni. Global Voices imekuwepo pale wakati mapinduzi yalipotokea, wakati tawala za kidikteta zikianguka, na matokeo ya matumizi ya mtandao yaliposambaa katika miji na mitaa ya wachangiaji wetu wanaoripoti kutoka duniani kote.
Iran: Yu Wapi Mwanafunzi Mwenzangu?
Several empty chairs in Iran's universities were formerly occupied by students who have now vanished or been expelled. This year Tahkim Vahdat, a leading student protest group, called for an “Empty Seat Campaign” on December 7 to remember the victims of religious and government repression in universities.
Zimbambwe: Hasira wakati Mzee Mugabe Anapowania Uchaguzi wa 2012
Chama cha ZANU –PF (Zimbabwe African National Union - Patriotic Front) kimempitisha Robert Mugabe kuwa mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao. Kama uchaguzi utafanyika mwakani, Mugabe atakuwa na umri wa miaka 88 na atakuwa Mwafrika wa pili mzee zaidi kugombea katika uchaguzi wa rais. Kupitia Twita na Facebook wa-Zimbabwe wameonyesha hasira na kutokuamini kilichotokea.