Habari kuhusu Video kutoka Januari, 2013
Uchafuzi wa Hewa wa Kutisha Jijini Tehran Waanikwa
Uchafuzi wa hewa umekuwa adui wa umma kwa mamilioni ya watu wa Tehran kwa miaka mingi sasa. Mapema mwezi huu, Wizara ya Afya ilitangaza kuwa, mwaka uliopita, zaidi ya watu 4, 400 walipoteza maisha kwa sababu ya uchafuzi wa hewa huko Tehran, mji mkuu wa Iran.
“Wanasemaje Bamako?” Mazungumzo na Awa anayeishi Mali
Anne Morin na Awa Traoré wanabadilishana mawazo kuhusiana na maisha ya kila siku mjini Bamako, ujira usiokidhi mahitaji, gharama za maisha na hali ya kisiasa isiyotabirika wakati huu ambapo vita vinanukia nchini humo.
Mwaka Mpya na Mienendo ya Zamani Nchini Bahrain
Wakati nchi mbalimbali ulimwenguni kote zikiukaribisha mwaka mpya kwa fataki na shamrashamra, serikali ya Bahraini iliandaa utaratibu wa aina yake kwa waandamanaji nchini humo. kwa bahati, watumiaji wa mtandao wa intaneti walikuwa tayari, kuonesha na kuweka kumbukumbu ya baadhi ya matukio kwa ajili ya kushuhudiwa na sehemu nyingine yote ya ulimwengu.