Habari kuhusu Video kutoka Machi, 2010
Mali: Vitambaa Vyasuka Nguzo za Uchumi na Utamaduni
Kwa kupitia video, tunaona na kujifunza kuhusu umuhimu wa utamaduni na ongezeko la kiuchumi ambalo utengenezaji vitambaa huwapa baadhi ya watu na mashirika nchini Mali. Vikundi vya wanawake, wasanii na watalii wote wananufaika na utamaduni huu wa kutia rangi vitambaa na upakaji rangi kwa kutumia matope.
Video: Tetemeko la Ardhi Chile Kwa Kupitia Macho ya Raia
Wakati siku inakaribia kuisha, video zaidi za tetemeko la ukubwa wa 8.8 ambalo liliikumba Chile majira ya saa 9.30 usiku zinajitokeza. Tetemeko hilo, ambalo halikuathiri maeneo ya bara pekee kwa njia ya kusogea sogea kwa ardhi, kadhalika lilisababisha mawimbi ya tsunami mabyo yalizua tahadhari katika eneo zima la Pasifiki huku mataifa mbalimbali yakijiandaa kwa mawimbi hayo pindi yatakapofika kwenye fukwe zao.