Unapenda wimbo gani wa kulalia?

Baby sleeps

Mtoto mchanga akiwa amelala kwenye hospitali ya Southern Luzon, Ufilipino (2009). Picha na Oliver Belarga – CC BY-NC-ND 2.0

Hadithi hii ya April Peavy iliyoandikwa kwa ajili ya The World ilionekana kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa PRI.org mnamo Aprili 7, 2014 na inachapishwa tena kwenye Global Voices kama sehemu ya makubaliano ya kushirikiana maudhui.

Wazazi wapya duniani kote hukabiliana na tatizo linalofanana: kuwafanya watoto wao wapate usingizi. Na kwa bahati njema, kuna ufumbuzi unaofanana: wimbo wa kulalia!

Lakini inaonekana kuwa si tu kwamba nyimbo la kulalia zinawasaidia watoto kupumzika, lakini pia zinawasaidia watu wazima, hali kadhalika, anaeleza mwandishi Kathy Henderson, aliyekusanya nyimbo za aina hiyo kutoka kila kona ya dunia alipokuwa akiandaa kitabu chake cha watoto kiitwacho, Hush, Baby, Hush [Tulia, Mtoto, Tulia]. Anasema nyimbo hizo tulivu zinawasaidia wazazi “kukabiliana na hali ya kusumbuka na watoto, au wanapojikuta hawawezi kuwafanya walale, au hata katika nyakati ambazo wao wenyewe wamechoka.”

Jina la kitabu cha Henderson kimetokana na wimbo wa ijamaika iitwao “Hush Baby Hush,” ambao toleo lake limerekodiwa na studio ya The Kitchen Sisters.

Mwandishi anasema nyimbo hizi zina sifa inayofanana. Zote zina muziki na maneno. Muziki una “ala nyororo” sambamba na mapigo ya taratibu.

Lakini mashairi, anasema, yanaweza kuhusu chochote -na yanabeba ujumbe wa aina mbalimbali za kihisia na mwonekano.

Kuna nyimbo za hasira, kukatishwa tamaa, na ucheshi. Henderson anabainisha kuwa zipo nyimbo kuhusu “chakula, familia, majinamizi, watoto wasumbufu” na mambo mengine mengi.

Kwenye wimbo wa Kituruki unaoitwa “Dandini Dan,” moja wapo ya beti unahusiana ndama wanaoenda kwenye bustani na mwenye shamba anawafukuza.

https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=gNWGnTtKZwA

Nyimbo za aina hii huimbwa katika hali za aina zote, si tu wakati mtoto anatafuta usingizi. kwa mfano, akina mama wakati mwingine wanaimba wakiwa wakifanya kazi, ili kuwafanya watoto wao watulie na kuwapa nafasi ya kufanya kazi.

Henderson anakumbuka wimbo wa zamani kabisa una historia ndefu na kusema watafiti wamegundua nyimbo za aina hiyo kupitia fasihi za kale zinazofahamika.

Mtandao wa PRI unakusanya na kusambaza nyimbo hizo kutoka duniani kote kwenye zana yetu, The World's Lullabies. Unaweza kusikiliza na kutuambia unapenda zipi. Unataka kututumia zile unazozipenda? Zipandishe ziwe kwa mfumo wa sauti na video -au kwa kubofya kitufe na kusikiliza kwenye kifaa chako cha mkononi au kompyuta.

April Peavey ni mtayarishaji na mwandaaji wa kipindi cha The World kinachoendeshwa na PRI.

Jifunze na tutumie nyimbo kwenye mtandao wa PRI.org

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.