Waziri Mkuu Mwanamke wa Kwanza wa Jamaica Astaafu Akisifiwa, Akikoselewa — na Mjadala wa Nani Atakuwa Mrithi Wake

Waziri Mkuu wa zamani wa Jaimaica, Portia Simpson-Miller, alipohudhuria sheria za kupitisha ubunifu utakayowakilisha kumbukumbu la utumwa huko Umoja wa Mataifa (kwa wadhifa wake kama Waziri Mkuu). Picha na kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, CC BY-NC-ND 2.0.

Mnamo Juni 29, 2017, Waziri Mkuu mwanamke wa kwanza wa Jamaica, Portia Simpson-Miller, alitoa hotuba yake ya mwisho ndani ya bunge. Kwa umri wake wa miaka 72 anafika mwisho wa safari yake ya siasa za uwakilishi.

Simpson-Miller amekuwa katika shinikizo la kujiuzulu kama kiongozi wa upinzani tangu pale Chama Cha Wananchi (PNP), chini ya uongozi wake kiliposhindwa katika uchaguzi mkuu hapo Februari 2016. Waziri wa Zamani wa Fedha, Peter Phillips, alirudishwa bila kupingwa kama kiongozi wa chama, na aliapishwa kama kiongozi wa Upinzani hapo Aprili 3, 2017.

Bi. Simpson Miller alifunikwa na hotuba mbali mbali toka  kwa wenzake wa pande zote mbili bungeni katika bunge la pamoja lililokaa hapo June 27, ambapo alielezewa kuwa mshindi kwa maskini. Akiwa na asili ya mtu wa mashambani, safari yake ya kisiasa kama mwanamke mada nyingi zilikuwa za kumpongeza na kumsifia kwa ujasiri aliouonesha katika changamoto mbalimbali alizokutana nazo mara kwa mara. Hata hivyo, uongozi wake ulileta maswali mara kwa mara katika vipindi vyake viwili kama Wazir Mkuu, na hata alivyoondoka katika jukwaa la siasa bado yuko na vizuizi vyake.

Mburudishaji mkubwa Tanya Stephens alitumia mtandao wa Facebook kufikisha ukosoaji mkubwa dhidi ya kumbukumbu ya Simpson-Miller:

Kusikia watu wanalalamikia kuondoka kwa Portia ni kama kuona watu wakimpongeza mbakaji wangu kwa kuwa mwanaume mwema….Portia sio mtu mzuri. Anafahamu hilo. Licha ya uwakilishi usioridhisha na udhalilishaji hana akili ya kiwango kinachooneshwa na umma, alikuwa mtu mbaya na asiye na utu ndani yake aliyeweza kuukuwadia vyema unafiki wa Wa-Jamaica. Nimefurahi kumuona akiondoka. Siko peke yangu. Kuondoka kwema.

Stephens aliwajibu Wajamaica wengi waliokerwa na maneno yake kirahisi tu kwa kusema:

Inahitaji ‘ujasiri’ kumkosoa MTUMISHI WA UMMA ni hatari.

Ikichukuliwa ni vita vya maneno, mwanaharakati wa kijamii Damien Williams alisema:

Kufananisha shamrashamra &  mapenzi mema kwa PSM [Portia Simpson-Miller] na zile zinazotolewa kwa mbakaji SIO ukosoaji wa kiwango chake, ushindani au maoni juu ya kushindwa kwake ila kwa uwazi na kwa urahisi kabisa hilo ni shambulio CHAFU na binafsi. Hata hivyo, kumtetea PSM kwa njia ile ile nayo pia ni uhuni vile vile. Ubakaji HAUWEZI kubezwa au kutumiwa kusababisha maumivu au kufidiwa. Tunaweza kukinzana bila kudhalilishana. Mara zote tumekuwa wa ajabu sana halafu tunatumia kama kisingizio cha uhuru wa kujieleza. KMT [Busu Meno Yangu]

Kwa Upendo anafahamika kama “Mama P,” Simpson-Miller alikuwa mwenyekiti katika ngome ya changarawe ya jimbo la Kusini Magharibi St. Andrew kwa zaidi ya miongo minne. Ni sehemu ya ndani ya mji lililo na miundo mbinu mibovu, ukosefu wa ajira na umaskini. Mwandishi wa Makala Martin Henry aliandika:

Portia Simpson alikuja katika siasa za uwakilishi kwa ngazi ya bunge mwaka 1976 wakati siasa za ukabila na mabaya yake, vurugu za kisiasa zilikuwa za hali ya juu. Hali ya hatari ilitangazwa na serikali mwaka huo, ikiwa ni matokeo ya vurugu zilizosababishwa na kampeni za uchaguzi, ikisaidia diwani kijana wa KSAC kushikilia nafasi ya JLP mpaka hapo ilipoonekana kuwa ni salama tena, na PNP haijawahi kushinda tangu kuundwa kwake hapo 1959. Kiwango cha asilimia 76 za ushindi wake hapo 1976 kimeendelea kukua kufikia kiwango cha idadi sawa na wapiga kura, hata pale wachache walipopiga kura kwa mgombea wa JLP.

Tangu 1976, vurugu za kihalifu, mauaji yakiongoza, imeendelea kuongezeka na Kusini Magharibi St Andrew ikichangia kwa asilimia nyingi.

Ndani ya wiki moja au mbili za kujiuzulu kwa Simpson-Miller kama mbunge, chama chake kimeanza kugubikwa kidogo kidogo na mkanganyiko na mpambano wa kisiasa juu ya mrithi wa jimbo lake. Hili liliripotiwa na kutolewa maoni na vyombo vya habari pamoja na mitamdao ya kijamii. Wa-Jamaica wanapenda fitna za kisiasa na wengi (hasa wale wenye maslahi na chama) hufuatilia kila jambo kwa hamasa.

Habari ilianza na kiroja– na mauaji– wakati Diwani Karl Blake (anafikiriwa kuwa ndie mrithi) alipojeruhiwa na msaidizi wake kuuawa kwa kupigwa risasi katika ofisi za jimbo lao. Blake, ambaye amepata nafuu, ameripotiwa kutokutaka kugombea nafasi hiyo tena.

Wakati Diwani Audrey Smith-Facey, ambaye anafanya kampeni kwa hashtagi #AudreyWetu, alitarajiwa kuwa ndiye mpinzani mkuu, maji yalivurugwa mno pale video ya Simpson Miller akimuidhinisha Meya wa zamani wa Kingston, Diwani Angela Brown-Burke, kuwa mrithi wake. Hii ilikuwa mshtuko kwa wengi kukiwa na maswali kama ilikuwa ni vizuri, kutolewa wakati kipindi cha uteuzi kikiwa kimepita, hili limekifanya chama kiingie katika mkanganyiko zaidi.

Kulingana na moja ya taarifa za habari, hata hivyo, wajumbe wa chama wamemkataa Brown-Burke. Wengi wangependa kumuona kijana machachari Damion Crawford, akichukua nafasi hiyo. Inaonekana Crawford hana mpango na nafasi hiyo ila hilo halimzuii kufurahia mzaha katika jambo hilo (akiwa amefungamanisha pembe zake na Brown Burke katika mitandao ya jamii mwaka 2015):

Crawford mwenyewe aliongeza:

Akiandika akijifanya amevurugikiwa:

Hata hivyo, baadhi ya wanahabari wanaufurahia msuguano ulio ndani ya chama:

#AudreyWetu haioneshi ishara ya kushidwa, huku ikitengenezwa kauli ya kejeli kuwa anatarajia kuwa “mwenye viwango”. Mjamaica mmoja mtumiaji wa Twitter alishangaa:

Sio la kufanywa kwa kupitiliza, Diwani Brown-Burke ametingwa na kampeni katika ukurasa wake wa Facebook, ikiwamo picha yake aliyopiga na “watu wake” jimboni kwake. Pia hapotezi muda wake kwa kuhariri picha ya jalada la ukurasa wake Facebook ili usomeke “Nayashukuru mapambano niliyopitia, maana bila hayo nisingekuwa na ujasiri nilionao!”

Baada ya mkutano wa baraza la watendaji wa chama, PNP sasa wamekubaliana kuitisha mkutano wa uteuzi ili kuamua kati ya wanawake hao wawili hapo Julai 30, 2017.

Swali linalobaki ni kuwa ingawa: Portia Simpson-Miller bado anataka abaki akijihusisha na watu wa Kusini Magharibi St. Andrew, ambao aliwaelezea kama “ngao yake ya chuma”katika hotuba yake ya kuaga?. Labda hilo linategemeana na mwanamke atakayemrithi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.