Zoezi la Historia Lililotolewa Shuleni Kuhusu Namna ya Kufundisha Utumwa Lazua Mzozo Jamaica

Mtumwa akivuliwa nira ya utumwa nchini Jamaica, kati ya 1875 na 1940. Picha ya Wikimedia Commons; Picha na Ashley Van Haeften, CC BY 2.0.


Shule ya Hillel , ni shule ya binafsi iliyopo upande wa juu wa Kingston ambayo hivi karibuni ilikuwa ni kituo cha mdahalo wa zoezi la historia lililowataka wanafunzi wa darasa la tisa kubuni mtindo wa adhabu ya mtumwa.
Mawimbi ya hasira mtandaoni yalianza kupitia Facebook, na polepole yaliongezeka kupitia mtandao wa Twita ambapo malumbano yalianza kuhusu historia, utumwa, mbali na matabaka ya jamii lakini yaliyodumu kwa muda mfupi. Malumbano hayo yaliacha maswali mengi kuliko majibu hasa kuhusu namna gani kipindi kibaya katika historia ya Jamaika kinaweza kufundishwa.
Pia, zoezi liliwataka wanafunzi kujadili aina ya adhabu waliyochagua kama mfano wa ustaarabu wa Ulaya kwa madai kuwa uthibitisho wa waafrika kuwekwa utumwani ni kukosa ustaarabu wao. Maelezo ya zoezi hilo la historia yalitumwa pia kupitia Facebook , pamoja na maoni:

Shule ya Hillel katika nchi ya Jamaica imewauliza wanafunzi kutumia ubunifu wao kuelezea kwa kuandika maumivu yaliyotokea kipindi cha utumwa. Lengo ni kupanua mtazamo wa mwanafunzi juu ya hali hiyo. Kama kweli hivyo ndivyo;
1) Simamisheni somo hilo mara moja.
2) Watoto wa jamii ya wakulima wa mashamba makubwa ya zamani wanaweza kufundishwa maridhiano, ukweli na namna ya kumaliza ugomvi na sio kuhadithia na kufikiria uovu.
3) Unawafundisha watoto kuwa mabwana wa watumwa wakati hali hiyo inawafaa wazungu wa jamii ya kibepari ya mwaka 1764. Hii inaadhiri heshima ya jamii nzima ya mwaka 2018 inayoendelea kustaarabika.
4) Waombeni wakurugenzi wa kipindi cha kampeni ya upendo waje kuongea na wanafunzi wenu kuhusu madhara ya hadithi za vurugu kwa watu wanaoshawishika haraka na kuhitajika kubadilisha mawazo hayo na mawazo mapya ya upatanifu na kuoneana huruma .

Mtumiaji wa Facebook aliyetuma zoezi hilo alieleza majibu yaliyotoka shuleni juu ya jambo hili:

Nina nakala ya zoezi kwenye karatasi na nimepata nakala nyepesi ya jibu lake kutoka shule:
‘Kuna majibizano makubwa na nitaelezea kwa nini. Mradi unalenga kuweka historia katika mtazamo. Wakati watoto wakubwa walipokuwa shule ya Hillel walijifunza mbinu za kufundisha utumwa kwa kukariri yaani kuhadithia vitu halisi tu. Leo, mbinu za kufundisha historia zimebadilika. Ukweli wa somo haujabadilika isipokuwa namna ya kulifundisha. Wanafunzi wanahimizwa ikiwezekana kuwa na mitazamo yenye urari.’

Shule ya Hillel ni taasisi isiyo ya kidini na isiyozalisha faida ambayo inatoa elimu kuanzia chekechea hadi sekondari ya juu. Ilianzishwa mwaka 1969 na Umoja wa watu wa Israel wanaoishi Jamaica. Ni shule inayoheshimika kwa kuelimisha wasomi wengi wa Jamaika. Ada yake ni kubwa sana kuliko shule za serikali na hata mitihani yake pia. Inatoa kozi kwa ajili ya kufanya mtihani wa mwisho wa Elimu ya Sekondari kimataifa na inatambuliwa na chama cha elimu ya juu na vyuo vya kati kusini mwa Jamaika. Katika kujifunza hutumia mbinu za zamani kwa kiasi kidogo, na kauli mbiu yake ni “kujifunza ili kuishi”. Kutokana na tovuti yake, malengo yake ni kuandaa mwanafunzi mwenye fikra wazi zaidi, mdadisi, mwenye kuthubutu, mwenye fikra urari, na uwezo mpana wa kufikiri.”

‘Wanafunzi werevu waliopewa zoezi wangeandika kuwa hakuna uthibitisho wa utumwa ‘

Hata hivyo maelezo ya shule kuhusu zoezi hilo hayakuweza kuzuia hasira ya watuamiji wa mtandao wa twitter ambao walikuwa hasa wamekasirikia matumizi ya neno “uthibitisho”:

Kitu nilichokipenda kuhusu namna historia ilivyofundishwa katika shule za Jamaica ni kutokujaribu kuthibitisha matendo yaliyofanywa na wakoloni. Hasa katika Dunia ya leo ambapo kumeinuka mawazo ya ki-Nazi ni hatari kuwauliza wanafunzi wengi wa kizungu kuthibitisha utumwa

Yakiwa kama majibu, kituo kimoja cha redio kiliripoti haraka maoni ya Profesa maarufu wa Historia:

HABARI: UWI Verene Shepherd Profesa wa hitoria ya jamii anasema wanafunzi werevu waliotakiwa kutoa uthibitisho wa utumwa katika shule ya Hillel, wangeandika kwamba ‘hakuna uthibitisho wa utumwa’

Mmoja wa watumiaji wa mtandao wa Twitter alipendekeza kwamba “bakra masters” (yenye maana ya mabwana wa kizungu wa watumwa) wanapandikiza mtazamo wao kuhusu utumwa shuleni:

Historia yetu inafundishwa kupitia macho ya mabwana wa watumwa na chanzo chake ni biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki. Sasa mabwana wa watumwa wanatuhimiza kutosoma historia kutokana na mitazamo yao bali kufikiria jinsi walivyofanya. Hii ni aibu.

Kulikuwa na mashambulizi mengi yaliyoelekezwa kwenye shule hiyo…..na wanafunzi wake. Hata hivyo mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii alikanusha uelewa uliopo kuwa shule hiyo ni ya wazungu tu:

Mtumiaji mwingine kupitia mtandao wa Twitter alichangia picha yenye maneno yaliyosemwa na Dr. Martin Luther King mwaka 1965 akiwa ziarani Jamaica, alikisifia kisiwa hicho kwa kutokuwa na ubaguzi wa rangi, alisema:

Kitu nilichokipenda kuhusu namna historia ilivyofundishwa katika shule za Jamaika ni kutokujaribu kuthibitisha matendo yaliyofanywa na wakoloni. Hasa katika Dunia ya leo ambapo kumeinuka mawazo ya ki-Nazi ni hatari kuwauliza wanafunzi wengi wa kizungu kuthibitisha utumwa

Punda wa mwaka amekwenda shule ya Hillel kutokana wajibu wa waelimishaji wa fikra kwa baadhi ya vijana wa Jamaika miongoni mwetu. Gumu! – Wanafunzi hamuwafundishi kuhurumiana na mnawauliza kuthibitisha utumwa; kwa kueleza adhabu ambayo wangetumia;

Je, ni kujaribu ‘kutenganisha fikra iliyopotoshwa ambayo ilitumiwa kuthibitisha utumwa ‘?

Kwa kujua ukubwa wa kosa , shule iliomba msamaha katika kauli iliyotolewa na bodi ya wakurungenzi na taarifa hiyo kutumwa kwenye mtandao na vyombo vya habari vikubwa lakini tayari mjadala ulikuwa umegeukia swali la matabaka ya kijamii na mbari katika Jamaica:

Mwalimu mwingine wa heshima alitoa tahakiki kali, ambayo ilitumwa kama picha kupitia mtandao wa Twita . Mwalimu wa Kiingereza alihitimisha hivi:

Mwalimu, umekosea, na nina shaka hii ni mara ya kwanza kwa sababu haujatumia vizuri lugha ya Kiingereza kuunda swali vizuri ili wanafunzi wachunguze kauli zinazopinga au kukubali utumwa kwa kina bila kuliacha darasa lako likifikiri kuwa kulikuwa na faida katika utumwa wa waafrika.

Baadhi ya watu walieleza kuwa historia ya ….na “uthibitisho wa” … – utumwa ulikuwa mara kwa mara ukifundishwa katika shule za Jamaika, si katika njia hii. Mwingine alikumbuka somo lake mwenyewe la historia katika kisiwa cha Karibi akiwa sekondari ya juu alisistiza kuwa zoezi kama hili ni la kawaida:

Sioni tatizo juu ya zoezi la historia lililotolewa katika shule ya HilIel. Je, tatizo ni zoezi au ni shule ambapo zoezi limetolewa? Nilifanya zoezi la historia katika kisiwa cha Karibi na nilitakiwa kuandika habari kuhusu mantiki iliyopo katika uthibitisho wa utumwa na adhabu iliyotumika.

na hakukuwepo na hasira tulipofanya hivyo. Kujifunza mambo yote ya utumwa ni muhimu. Sio tu maasi ndiyo yatufanye tufurahi kwa ufahari tunapojifunza juu ya babu zetu lakini pia mwelekeo wa kufikiri ambao unawaweka katika nafasi ya kwanza.

Mwanasheria wa haki za binadamu, ambaye hutetea ulipaji fidia za utumwa alichambua madhumuni ya zoezi hilo:

Hili zoezi katika shule ya Hilllel linaonekana lilikuwa linajaribu kutenganisha fikra potofu ambayo ilitumika kuthibitisha utumwa kwa miaka zaidi ya 400. Wamiliki wa watumwa waliowengi walienda kanisani kila Jumapili na kujiita wakristo, na bado hawakuweza kuliona hili katika fikra zao.

Hapa kuna swali la kufafanua; Kama wazungu walifikiriwa kuwa ni wastaarabu na waafrika sio wastaarabu. Je, ni ustaarabu gani kwa mateso ya kikatili waliyofanyiwa wafungwa?

‘Je, shule binafsi zinaruhusiwa kufundisha chochote wanachotaka?’

Je, zoezi hili lingekubalika katika muktadha mwingine? Watumiaji wengi wa mtandao wa Twita waliuliza:

Je, kwa zoezi hili, shule ya Hillel ingeweza kutoa zoezi la kubuni njia walizotumia wanazi wa kijerumani kuteketeza wayahudi katika vita kuu ya pili ya dunia?

Kwa hiyo, ni jambo gani baya kuhusu shule ya Hillel? Raia wa mtandaoni walianza kuzungumzia uwajibikaji katika uandaaji wa mtaala. Chombo cha habari kijulikanacho kama Personality kilitwiti:

Nimeenda mbali zaidi ya shule ya Hillel. Nauliza ni nani ambaye anayehakiki maandalio ya masomo shuleni? Je, shule binafsi zinaruhusiwa kufundisha lolote wanalolitaka? Je shule za Jamaica hazipewi leseni ili zifanye kazi chini ya mwongozo fulani ili kuendana na sera ya taifa ya elimu na utamaduni?

Wengine walikuwa na mtazamo mpana katika mazungumzo kwa kutafakari juu ya siku mpya ya utumwa:

Inawezekana utumwa umetoweka lakini imani potofu iliyosababisha kuwepo kwa utumwa bado bado imani hizo zipo na hasa imani juu ya wazungu ambao walifurahia utamu katika chai yao wakati wakigeuka vipofu kwa mateso ya kutisha waliyoyafanya.

Leo tuna makumi elfu ya watoto katika Afrika wanaofanya kazi katika hali ya karaha katika machimbo ya chuma ambayo hutumika kwa ajili ya betri za simu za mikononi au kuokota kokwa za kakao kwa ajili ya chokoleti ni kama karne ya 18 wakati ambao wakoloni wa kizungu walikuwa wanafurahia utamu katika chai yao, walaji wengi hawajali.

Baada ya hasira kupitia vyombo vya habari, swali linabakia: Ni jinsi gani maumivu ya historia ya visiwa vya Karibi, ukoloni pamoja na utumwa vitafundishwa katika ulimwengu huu wa kizazi cha vijana? Kwa jaribio hili la hivi karibuni kuhusu “uvumbuzi”, hata kama unalengo zuri ukifanya maamuzi kwa upinzani unaweza ukawa umesababisha madhara zaidi ya mazuri.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.