M-Misri Atumia Mtandao wa YouTube Kupinga Kutumikia Jeshi kwa Lazima

Mwanaharakati wa Misri ametumia mtandao wa YouTube kuelezea anavyopinga utaratibu wa kulitumikia jeshi kwa lazima kwa raia wenye umri wa miaka kati ya 18 na 30.

Katika barua pepe aliyoituma kwa Global Voices mtandaoni, Adam anaandika:

Mimi ni Mmisri mwangalifu ninayepinga kwa nguvu zote utaratibu wa kulitumikia Jeshi la Misri lazima kwa sababu nachukia vita na ghasia. Nilirekodi video hiyo kwa lugha ya Kiarabu na kuitafsiri kwa kiingereza. Natumaini mtaiweka katika matangazo ya idhaa ya televisheni yenu ili Wamisri na dunia yote iweze kujua maoni yangu kwa sababu watu kama mimi tunaopinga kujiunga na jeshi kwa lazima hatupewi nafasi ya sauti zetu kusikika kwenye vyombo vya habari. Ni matumaini yangu kwamba mtanisaidia kwa sababu nataka Wa-Misri wawe huru kutoka utawala wa kijeshi na utawala wa dini. Naunga mkono demokrasia ya Magharibi.

Katika video hii, tafsiri ya maandishi katika lugha ya Kiingereza, Ahmed (Adam) anasema:

Mimi ni Ahmad (jina la utani Adam) kutoka Misri. Nitakueleza namna utaratibu wa kulazimisha kutumikia jeshi unavyofanyika nchini Misri. Napinga kwa nguvu zote utaratibu huu, na ninakataa kutumika katika Jeshi la Misri kwa sababu ni jeshi la jinai linalowauwa maelfu ya waandamanaji na watu wasio na hatia katika barabara ya Mohamed Mahmoud na Tahrir Square jijini Cairo na maeneo mengi katika Misri.

Anaongeza:

Kutumikia jeshi kwa lazima ni udhalilishaji, utumwa, na kazi ya kulazimishwa kwa maelfu ya Wamisri maskini ambao kila mwaka wanalazimishwa kufanya kazi katika biashara binafsi na mashamba ya majenerali wa jeshi la Misri bila malipo yoyote au mshahara. Askari yeyote ya Misri [ambaye] ametumikia katika jeshi anajua vizuri sana mikopo mikubwa majenerali wa jeshi inayoingizwa kwenye akaunti zao za benki. Pia, majenerali wa jeshi wanamiliki mali halisi ya mali isiyohamishika waliyoipata kwa njia haramu. Wanaiba utajiri wa nchi na mali.

Adam anaelezea:

Kulitumikia jeshi kwa lazima ni utaratibu usiokuwepo kokote kwa ajili ya maendeleo, iwe kwenye nchi yoyote ya Magharibi, wala Marekani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.