Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Malaysia
Filamu Yaonesha Namna Kabila Dogo Linavyojaribu Kuwazuia Wakata Misitu Kuharibu Mazingira
Sunset Over Selungo ni filamu ya dakika 30 inayoonesha namna kabila la wenyeji la Penan linavyopigania kutunzwa kwa misitu ya asili kwenye kisiwa cha Borneo nchini Malaysia. Borneo ni kisiwa kikubwa zaidi barani Asia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji huru wa filamu wa Kiingereza, Ross Harrison
Je, Ujumbe wa Shirika la Ndege la Singapore Baada ya Ndege MH17 Kuanguka Haukuwa wa Kiugwana??
Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita: Customers may wish to note that Singapore Airlines flights are not using Ukraine airspace. — Singapore Airlines (@SingaporeAir) July...
Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine
Wakati kukiwa na hisia zinazozidi kuongezeka kufuatia kuanguka kwa ndege nchi Ukraine, matamshi kadhaa yaliyotolewa na watu maarufu Moscow na Donetsk yamevuta hisia za watu
Waziri Mkuu wa Zamani wa Malayasia Aitaka Boeing Kuwajibika kwa Ajali ya Ndege MH370
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Mahathir Mohamad ameitaka Boeing kuwajibika kufuatia tukio la kupotea kwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia yenye namba MH370. Hivi ndivyo alivyoandika kwenye blogu yake: Boeing ndiyo imetengeneza ndege hii. Boeing lazima waeleze inakuwaje njia zote za kuifuatilia mwenendo wa ndege hiyo ziweze...
Kuumaliza Umasikini Nchini Malaysia
Kikundi cha Saya Anak Bangsa Malaysia kinashinikiza kupitishwa kwa Sheria ya Ujumuishi wa Kijamii ili kutatua tatizo la umasikini nchini Malaysia: Maelekezo yatokayo juu kuja chini yanaonekana kutokufanya kazi pamoja na madai tofauti ya serikali. Ili misaada ifanye kazi kweli, basi iende kupunguza ‘maumivu binafsi ya mfukoni’ kwa sababu kila...
Ufuatiliaji wa Upendeleo Kwenye Vyombo vya Habari Nchini Malaysia
Tessa Houghton anashiriki matokeo ya utafiti ambao ulifuatilia upendeleo katika vyombo vya habari nchini Malaysia wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 13 miezi michache iliyopita: Wananchi wa Malaysia ambao walitegemea Kiingereza na Bahasa magazeti ya Malaysia na/au televisheni kama chanzo cha vyombo vyao vya habari wakati wa kampeni ya GE13 hawakutolewa...
Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini
Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na...
Kufilisika kwa Watu nchini Malaysia
iMoney.my wametengeneza mchoro unaoelezea takwimu za kufilisika nchini Malaysia. Wastani wa matukio 20,000 ya kufilisika yamerekodiwa mwaka 2012 hiyo na maana kwamba wa-Malaysia 53 wanafilisika kila siku.