Habari kuhusu Elimu

Changamoto za Elimu kwa Karne ya 21

  30 Mei 2014

Mikel Agirregabiria kwa kujifunza kutoka kwenye filamu Dead Poets Society aliweza kubainisha [es] mahitaji ya sasa ya elimu: Elimu katika karne ya 21 yahitaji kushughulikia masuala ambayo hayakuwa bayana siku za nyuma, kama vile wapi unapotaka kuishi au kufanya kazi, kwa kutumia lugha gani au kwa utamaduni upi unaweza kujisikia...

Maktaba na Utamaduni Huru

  17 Mei 2014

Blogu kutoka Parque Biblioteca Tomás Carrasquilla – La Quintana, huko Medellin, Colombia, inaelezea [es] msaada wake kwa utamaduni huru. Baada ya kueleze namna ya kuleta utamaduni wa uhuru [es], blogu hiyo inaelezea jinsi inavyoweza kufanya kazi inayofanana na maktaba: Maktaba za umma zaweza kujifunza katika uhuru huu wa kubadilishana taratibu...

Bob Marley – Ni Mungu Mpya wa Vijana wa Bhutan?

  29 Aprili 2014

Bob Marley ghafla amegeuka mungu miongoni mwa kizazi kilichochanganyikiwa. bendera ya Rastafari, ikiwa na ama Bob mwenyewe au jani la bangi, inapatikana kokote. Kwa mtu aliyekufa mwaka 1981 na kuendelea kutawala akili za watoto wanaonekana kuwa na akili tena wa karne ya 21 ni jambo gumu kuamini. Passang Tshering, Mwanablogu...

Mradi Wa Kutumia Simu za Mkononi Kuhamasisha Usomaji

Lauri anaandika kuhusu mradi uliopo Afrika Kusini, Mfuko wa Usomaji wa FunDza, unaotumia teknolojia ya simu za mkononi kuhamasisha tabia ya kusoma kwa watoto: Kinachofurahisha, hata hivyo, ni pale Waafrika wanapopata majibu ya kiubinifu kwa matatizo yao. Mradi wa FunDza ni mfano moja wapo. Simu za mkononi zimeenea sana nchini...

Utafiti wa Wenyeji katika Chuo cha Bahamas

  3 Aprili 2014

Akifuatilia posti yake kuhusu “ujinga wa kupunguza bajeti kwa Chuo cha Bahamas”, Blogworld anasema: Si tu kwamba chuo hicho ni taasisi ya taifa ya elimu ya juu, lakini ndio taasisi pekee ya umma kwa wenyeji ambayo inahusiana na aina yoyote ya utafiti unaoendelea katika nchi ya Bahama.

Katika Kutetea Lugha za Malawi

Kufuatia uamuzi wa serikali ya Malawi kuanza kutumia Kiingereza kama lugha ya mawasiliano kuanzia darasa la kwanza, Steve Sharra anatetea lugha la asili na anajenga hoja yake katika kutetea matumizi ya lugha zaidi ya moja: Walimu na wahadhiri katika shule zetu za sekondari na vyuo vikuu wanashuhudia mwenendo wa mambo...