Habari kuhusu Elimu kutoka Oktoba, 2008
Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo
Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.
Madagascar: Kuishi ughaibuni hubadili uhusiano
Katika makala iliyochapishwa mwezi Machi, wachumi William Easterly na Yaw Nyarko wanaeleza kwamba katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara, kiasi cha fedha kinachotumwa na wahamiaji wanaotoka bara hilo...