Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Aprili, 2010
India, Pakistani: Hekaheka za Sania-Shoaib Zaendelea
Utata wa harusi ya Shoaib Malik na Sania Mirza unaendelea huku vyombo vya habari vikichochea hekaheka na mamilioni ya watu nchini India na Pakistani wanaendelea kuzama katika habari hiyo. Wakati wapenzi hao wanajiandaa na harusi na kuvishinda vikwazo, sehemu nyingine mashambulizi yanaendelea.
Piga kura kuchagua “Blogu Bora Zaidi”
Upigaji kura mtandaoni umeanza kwa ajili ya Tuzo ya Blogu Bora Zaidi inayotolewa na Deutsche Welle (Shirika la Habari la Ujerumani), moja kati ya mashindano ya blogu yenye hadhi kubwa kimataifa na blogu zilizotajwa kushiriki ni za lugha kumi na moja tofauti. Unaweza kuipigia kura blogu uipendayo hadi April 14, 2010.
Muziki Wenye Ujumbe – Video Mpya za Muziki Kutoka Tibet
Mradi wa kutafsiri Blogu uitwao High Peaks Pure Earth hivi karibuni umetupia jicho “muziki wenye ujumbe” kwa kutafsiri mashairi ya nyimbo za Tibet kutoka video za Muziki zilizowekwa kwenye mtandao....