India, Pakistani: Hekaheka za Sania-Shoaib Zaendelea

Utata wa harusi ya Shoaib Malik na Sania Mirza imewaamsha watu wa pande zote mbili za mpaka wa India na Pakistani. Huku kukiwa na mlipuko katika vyombo vya habari, inaonekana kuwa watu wan chi zote mbili wanashuhudia toleo la kiHindi la “papparazzi” kwani idhaa za Televisheni, magazeti na asasi nyingine vimewaandama, vimekusanya na kutoa kila chembe ya habari inayowezekana kuhusu harusi hii inayotarajiwa.

Mafuvu na mifupa vimemnyemelea Shoaib kwa kupitia “mke wake wa zamani” Ayesha Siddiqui, ambaye ilimbidi amtaliki rasmi ili kuumaliza utata. Madai na kesi inayomkabili nchini India hivi sasa vimeondolewa na familia ya Siddiqui baada ya malipo ya kiasi cha Rupia milioni 150 kama fedha za kumkimu aliyetalikiwa. Mapindo na mizunguko ya habari hii vimekuwa kama vurumai kwa vyombo vya habari na wazi wanablogu hawako nyuma sana. Ulimwengu wa blogu nchini India na Pakistani umewaka kwa mitazamo na midahalo, wengine wanafikiri kuwa hii ni ishara ya Amani inayokuja wakati wengine wanasema kuwa ndoa hii ni chanzo cha ugomvi wa baadaye.

Syed Zaki Ahmed wa Pak Spectator anafikiri kuwa ndoa hii na kelele zote ni nzuri kwa biashara:

Sasa katika hali kama hii wafanyabiashara wangebaki vipi nyuma. Wafanyabiashara nchini Pakistani wamejiunga na hafla kwani wanapata maagizo ya mamia ya maelfu ya fulana zenye picha ya Shoaib na Sania kuelekea harusi yao ambayo inatarajiwa kufungwa wiki ijayo siku ya tarehe 15 Aprili.

Blogu ya Wananiita Muislamu inatoa maoni kuhusu sababu zilizopelekea uamuzi wa Sania Mirza kuolewa na Shoaib Malik:

Je ni kipi ambacho Waislamu wa India watajifunza kutokana na uamuzi binafsi mno wa Sania? Ni hiki: Usiijutie Pakistani. Usiwe shuku zisizo na sababu kuhusu nchi hiyo kutokana na hofu ya kuitwa msaliti. Wewe sio msaliti.

Vyama vya kiHindu vyenye siasa za kulia, kuanzia Bajrang Dal mpaka Shiv Sena, waliufanya chakula uamuzi huo wa Sania. Na bado, mcheza tennis huyu anayevutia amejitosa. Kwa nini? Kwa sababu rahisi, ndani sana ya moyo wake, mapenzi yake kwa mPakistani na kuwa Mhindi havipaswi kwa lazima viwe vitu vinavyopingana.

Hata hivyo, Capricious anafikiri kuwa ndoa hiyo itaanguka:

* Sania Mirza amepata umaarufu wote, kujulikana, utajiri na nafasi ya kuwa kama nembo wakati akiwa na umri mdogo sana. Amekuwa ni kipenzi cha India, amekwezwa na kupendwa na Wahindi wote na kutangazwa na vyombo vya habari vya india na ulimwengu wote. […] Ni msichana huru. Tofauti na wasichana wengi wa Kiislamu katika Bara Hindi, hahitaji mume kwa ajili ya mkate na siagi (maisha). […] hali ya kutaka kuwapatia maisha familia ni jambo ambalo hukua na nafsi ya mwanamme yeyote, mtazamo pamoja na mamlaka yake. Inampa mPakistani Muislamu hasa fikra za hali ya chini. Mtizamo na fikra hizo siku zote hutaka jambo la ziada na upendeleo usio wa lazima kutoka kwa wake. Vitu ambavyo vitakosekana katika ndoa hii. Starehe ya kuwa “mume” Malik Shoaib hawezi kuipata.

Wakati kila siku inaleta habari kama Waziri Mkuu wa Pakistani atuma zawadi maalum kwa wanandoa, ukosoaji unaendelea sehemu nyingine. Baraza la Ulema la waSunni, kundi la wanazuo wa dini, imeripotiwa kuwa walitoa ‘fatwa’ (amri ya kidini) dhidi ya Sania na Shoaib kutokana na kutembea kwa uhuru na kwa kuishi pamoja kabla ya ndoa hiyo kupitishwa rasmi. Kuna hata usemi ulianzishwa kwenye twita kwa ajili ya muungano huu lenye alama ya #shoania

Tumeshuhudia ripoti za uvumi kwamba nikah yenyewe (uandikishaji ndoa) ulifanyika siku ya tarehe 9 Aprili. Lakini hakuna litakalokwisha mpaka hapo Sania na Shoaib watakaposema yamekwisha. Inaonekana kuwa vyombo vya habari vinachochea shauku hii na mamilioni ya watu katika nchi hizo mbili wanaendelea kuzama ndani ya mambo yote haya.

Ni wazi mambo haya uyataendelea mpaka tarehe 15 ya Aprili, huku nchi mbili zenye hisia kali zikiangalia mchezo wa filamu unavyojikunjua wenyewe katika maisha ya kweli.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.