Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Septemba, 2010
Karibeani: Kwa Heri, Arrow
Wanablogu wa Karibeani wanaomboleza kifo cha mmoja wa waasisi wa muziki wa soca katika kanda hiyo - Alphonsus Cassell, ambaye anayejulikana zaidi kama “arrow” – na ambaye kibao chake kikali, Hot, Hot, Hot kinapewa sifa ya kuutambulisha mtindo wa soca kwa kadamnasi duniani kote. Taarifa za habari zinathibitisha kuwa muimbaji huyo allikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda; rambirambi za wanablogu zimekuwa na mguso pia zinaelezea masikitiko binafsi...
Africa: Waafrika Wasimulia Kumbukumbu Zao za Utotoni
That African Girl ni blogu yenye mfululizo wa makala zilizoandikwa na Waafrika kutoka dunia nzima kuhusu maisha ya utotoni. Ni blogu inayoelezea kuhusu makuzi katika familia za Kiafrika na uzoefu wa kuishi katika tamaduni mbili.