· Mei, 2013

Habari kuhusu Sanaa na Utamaduni kutoka Mei, 2013

Ijue Mauritania kwa Jicho la Msanii wa Kireno

Msanii wa Kireno Isabel Fiadeiro anayeishi katika mji wa Nouakchott, Mauritania, ambako anachora na kuendesha maonyesho ya kazi ya sanaa. Fiadeiro vilevile huchora madhari kwa kuyatazama, hujaza blogu yake anayoiita Michoro nchini Mauritania na michoro ya maisha ya kila siku katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Global Voices ilizungumza na Fiadeiro kuhusu kazi yake ya sanaa na namna michoro yake ilivyomsaidia kuifahamu Mauritania.

Mfululizo wa Tamthilia ya Runinga ya Nchini Tanzania

The Team Tanzania (Timu Tanzania) ni mfululizo wa Tamthilia ya Runinga yenye kuzungumzia: […] Bi. Wito, mwalimu mahiri wa somo la uraia, anaigeuza kabisa mitazamo ya vijana makinda watatu anapowauliza maswali mazito mfano “Wewe ni nani”? vijana wale wenye umri wa miaka 16, waliofahamiana vyema tangu wakikua. Katika kuingia katika...